Dkt. Tulia ampa tabasamu mwananchi mwenye ulemavu kata ya Mwakibete

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole Mhe. Dkt. Tulia Ackson imemkabidhi kiti mwendo na mtaji wa shilingi laki tano (Tsh. 500,000/=) Mpoki Abraham anayeishi mtaa wa bombambili kata ya Mwakibete.

​
Mpoki (33) ni mjasiliamali mdogo mwemye duka la mahitaji ya nyumbani mwenye changamoto ya ulemavu wa miguu na mikono unaomfanya atembee kwa kutambaa, hivyo msaada huo utamsaidia kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kumuinua zaidi kiuchumi kwa kumuongezea mtaji.

​
Kupitia mbio za Bendera ya Upendo ya Tulia Trust iliyopeperushwa kwenye kata zote 13 za Jimbo la Uyole ilimbaini mhitaji huyo na kumuahidi kumpa msaada utakao muinua zaidi kiuchumi ili aweze kubadirisha maisha yake.



​
 
Sio kinyonge, naona Bw Mpoki anamiliki na ng'ora ya kupangisa kabisa mazeeee.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…