Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Oktoba, 2024 wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Grand Melia, Jijini Arusha uliofunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, akimuwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na Maspika na Wabunge kutoka zaidi ya nchi 19 za Barani Afrika, Dkt. Tulia alitumia fursa hiyo kuwashukuru wajumbe wa Umoja huo kwa kumchagua kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Aidha, aliwasihi washiriki hao kutumia uwepo wao mkoani Arusha kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika Mkoa huo ili kufurahia uzuri na urithi wa nchi ya Tanzania.