LGE2024 Dkt. Tulia awataka wananchi kuchagua viongozi wenye uwezo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya mjini, Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi kuchagua Viongozi wenye uwezo wa kushughulika na changamoto zao kwa urahisi ili kuweza kuwaletea maendeleo ya haraka katika jamii zao.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 26 Novemba, 2024 wakati akihitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Songwe zilizofanyika katika uwanja wa Uwanja wa Mwaka, Tunduma ambapo Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Novemba, 2024.

Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024


Amesemema kuwa, Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama pekee kinachojua changamoto zao na kinao uwezo wa kuzitatua kwakuwa kwa dhamana iliyopewa kupitia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweza kuzishughulikia hivyo ni vyema kuendelea kukiamini ili kuzimaliza zote.
 

SPIKA DKT. TULIA AWATAKA WANANCHI KUCHAGUA VIONGOZI WENYE UWEZO

Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi kuchagua Viongozi wenye uwezo wa kushughulika na changamoto zao kwa urahisi ili kuweza kuwaletea maendeleo ya haraka katika jamii zao.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 26 Novemba, 2024 wakati akihitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Songwe zilizofanyika katika uwanja wa Uwanja wa Mwaka, Tunduma ambapo Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Novemba, 2024.

Amesemema kuwa, Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama pekee kinachojua changamoto zao na kinao uwezo wa kuzitatua kwakuwa kwa dhamana iliyopewa kupitia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweza kuzishughulikia hivyo ni vyema kuendelea kukiamini ili kuzimaliza zote.
 

Attachments

  • GdUoVMxXwAAMBYC.jpg
    330.5 KB · Views: 2
  • GdUoVMwXYAAO5fY.jpg
    319 KB · Views: 3
  • GdUoVMwXsAAmIJv.jpg
    423.5 KB · Views: 3
  • GdUoVMyXAAAPS2R.jpg
    242.9 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…