Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mgombea ubunge jimbo la Uyole, jijini Mbeya, Dkt. Tulia Ackson, ameahidi kumalizia kazi aliyoianza ya kufanikisha upatikanaji wa maeneo kwaajili ya mafundi wa magari ambao hufanya shughuli zao maeneo ya magerejini kata ya Mwakibete.
Akiendelea na kampeni zake za kata kwa kata Dkt. Tulia amesema mwanzo baada ya kuwatembelea vijana hao alikutana na changamoto ya eneo la kazi na alianza kulishughulikia ambapo hadi sasa tayari kuna maeneo matatu yametengwa na jiji la Mbeya kwaajili ya gereji yaliyopo Nanenane, Mlimanyoka na Iganjo na sasa yanasubiri maelekezo ya kuanza kutumika.
Awali wakizungumza juu ya ufinyu wa maeneo mafundi hao wamesema sehemu kubwa ya gereji zao hufungwa kutokana na wamiliki wa maeneo wanayofanyia kazi kuuzwa na wamiliki wapya kubadili matumizi hivyo hubaki bila kazi jambo linalowarudisha nyuma kiuchumi.
Aidha vijana hao wamepongeza hatua zilizochukuliwa kwa kuwapatia eneo la nanenane ambalo wanaamini litakapo anza kutumika litawasaidi kukuza uchumi wao kwakua hakutakua na kuhama mara kwa mara kwa sababu ya wamiliki kuuza maeneo yao.
Hao wana ufinyu Je wale Machinga wa nchi nzima wanaofanya kazi barabarani ambao mlikuja na Sera zenu sijui za kuwahamisha / kupanga maeneo na wengine mpaka kuja na vijibanda eti wanawatengenezea !!!!
Niliona Morogoro wanazindua vibanda vya Machinga...
Hio ni vema na Haki... ila swali la kujiuliza tuna tatizo la mabanda au sehemu za kufanyia biashara ? Machinga Complex ilijaa au tulikosea wapi ?
Unaweza kusema ingawa frame / maduka yapo ila ni gharama Je Machinga wanashindwa kujichanga hata watano wakachangia frame (after all wamezoea kufanya kazi karibu karibu) si ni bora wakae kwenye nyumba...