Pre GE2025 Dkt. Tulia kuijengea nyumba familia yenye uhitaji Kyela, atoa msaada wa chakula na mavazi

Pre GE2025 Dkt. Tulia kuijengea nyumba familia yenye uhitaji Kyela, atoa msaada wa chakula na mavazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Taasisi ya Tulia Trust Chini ya Mkurugenzi wake ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson yapeleka Tabasamu kwa Familia ya Obed Ambonisye Mwalopale.

1741781985208.png

Nyumba ya Familia ya Obed Ambonisye Mwalopale
Mzee Mwalopale Mwenye Changamoto ya Ulemavu wa Miguu anaishi na Familia yake ya Watoto Wanne Katika Kijiji Cha Matema Kata ya Matema Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya amepatiwa Msaada wa Kujengewa Nyumba na Tulia Trust kutokana Changamoto ya Kukosa Makazi, Ujenzi unaotarajiwa Kuanzia Siku ya Jumatano ya Machi 12, 2025 na Kukamilika baada ya Siku 14.

Soma, Pia: Dkt. Tulia Ackson akabidhi nyumba kwa Mkazi wa Mbeya kupitia Tulia Trust

Nyumba anayoishi na Familia yake kwa Sasa haina Mazingira Mazuri Jambo linaloweza kuhatarisha Maisha yake hasa Wakati wa Mvua, Nje ya Kujengewa Nyumba wamepewa Msaada wa Mavazi na Chakula kwani Mahitaji hayo pia ni Changamoto kuyapata.

1741782045845.png

1741782066823.png
 
Kyela hakuna dhiki hiyo, labda kama wameamua kufanya siasa
 
Back
Top Bottom