johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia amemtaka Waziri wa Ujenzi kuangalia namna ya kuiwezesha TAZARA kuwa na treni ya umeme.
Dr. Tulia amesema Tanzania ni moja na Wananchi wa pande zote wanahitaji maendeleo hivyo Kanda ya Nyanda za Juu Jusini wamechoka kuwa washangiliaji.
Kadhalika Dr Tulia amelalamikia Jiji la Mbeya kutopewa hadhi na Huduma stahiki kama ilivyo katika majiji mengine na badala yake Mbeya imekuwa kama Halmashauri.
Tulia amesema miundombinu ya Mbeya ni mibovu sana na miaka yote wamekuwa wakipewa bajeti ndogo isiyokidhi chochote.
Dr. Tulia alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi.
Source: Bungeni