Dkt. Tulia spika wa bunge jitokeze hadharani ukemee jina lako kutumiwa na matapeli

Dkt. Tulia spika wa bunge jitokeze hadharani ukemee jina lako kutumiwa na matapeli

Mzalendo120

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
2,410
Wanajukwaa natumaini mnaendelea vizuri. Kwawale wenye changamoto nawapa pole na kuwaombea kwa Muumba ahueni ipatikane.

Nikienda kwenye mada nikwamba vipo vikundi au taasisi zinazojihusisha na mikopo tena kwakutumia majina ua viongozi wa chama na serikali na wafanya biashara wakubwa.

Miongoni mwazo ni Mo DewjiFoundation ,Tulia Ackson na ile ya Joketi.

Nimeamua kuzungumzia hii ya Tulia kwasababu kuna mtu ametapeliwa hela juzi lakini nikasema ngoja nione wanatapeli vipi.

Wakati ninachati nao wamesema nipige kitambulisho picha niwatumie pamoja na namba ya kupokelea hela zitakazo ingizwa.

Katika kuongea nao nikawaambia wanielekeze ofisi zao zilipo wakasema zipo Chamwino. Nikawaambia naweza kuwapelekea hela za awali za mkopo ili wanipatie kiwango ninachoomba? Wakajibu hapana wanafanya huduma online. Je hata kama nipo hapa jirani? Wanasema hapana wao ni online tu.

Baada ya hapo wanafanya videocall eti wanione. Unaweza ukajiuliza mtu anaesema usiende ofisini utumetu taarifa online lakini anataka kukuona videocall je nimzima huyo?

Kilichonishangaza zaidi juu ya matapeli hao nikufita sms zote walizonitumia. Je kwanini wamefuta?

Tulia Ackson hawa wanaotumia jina lako nimatapeli kama matapeli wenginetu. Usipo wakemea na kuomba jeshi la polisi likusaidie kuwasaka basi umewatuma na itakua unafaidika na huo utapeli.

Jipambanue wakatae hadharani hao matapeli au kama taasisi kweli niyako basi weka watu waadilifu hao waliopo nimatapeli wakubwa
 

Attachments

  • Screenshot_20240501-174724.png
    Screenshot_20240501-174724.png
    579.8 KB · Views: 5
  • Screenshot_20240501-174641.png
    Screenshot_20240501-174641.png
    550.5 KB · Views: 6
  • Screenshot_20240501-152954.png
    Screenshot_20240501-152954.png
    619.1 KB · Views: 4
  • Screenshot_20240501-174700.png
    Screenshot_20240501-174700.png
    600.3 KB · Views: 5
Upumbavu ni wewe mwenye shida ya mkopo halafu unaambiwa utowe pesa, wewe inakuingia akilini hiyo?
Hahaha! Mshikaji wangu alipingwa laki nne kwa ahadi ya mkopo wa milioni tatu! Jioni wanampigia video call wamechafua meza na bia.

Wanaitwa TALA na watu maarufu kina shilole, kitenge wanawatangaza. Ila jichanganye! Na IG comment section yao wanafunga.
 
Upumbavu ni wewe mwenye shida ya mkopo halafu unaambiwa utowe pesa, wewe inakuingia akilini hiyo?
Mbona hata kwenye ma Bank huwa wanataka pesa kwanza kabla ya kutoa mkopo? Mfano Gharama ya huduma, bima nk. NB , sitetei matapeli lazima watokomezwe.
 
Hahaha! Mshikaji wangu alipingwa laki nne kwa ahadi ya mkopo wa milioni tatu! Jioni wanampigia video call wamechafua meza na bia.

Wanaitwa TALA na watu maarufu kina shilole, kitenge wanawatangaza. Ila jichanganye! Na IG comment section yao wanafunga.
Yani nchi inawezi na hawaogopi kutumia majina hata ya viongozi. Au hata hao viongozi wanafaidika? Kwanini mtulie
 
Habari hiyo inadhihirisha utapeli wa Tulia Foundatio. Hivi nyie viongozi wa chama na serikali hamuoni aibu? Taasisi ya bunge hamuoni kichefuchefu?
Je hao wanaotajwa sio wanufaika wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu? Sasa Tulia anahusikaje hapo? Mbona mnalipwa hela za kufuru kisha mnaibia mafukara? Ikifika siku ya ibada eti nae anatoa sadaka. Sadaka ipi inayotokana na utapeli?

Hii ni aibu kwa chama,serikali na bunge
Screenshot_20240501-152954.png
 
Back
Top Bottom