Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za wakati huu,
Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na jitihada zako za kutafuta mafanikio katika maisha yako. Niseme tu ukweli kwamba ninaandika andiko hili nikiwa katika maombolezo ya msiba.Nina Misiba ya watu tofauti katika mazingira tofauti ambao walikuwa ni wateja wangu,rafiki zangu and role models wangu.Misiba hii inaniuma sana kwa sababu ya umri wao mchanga,maono yao makubwa,mafanikio ya makubwa lakini zaidi ni namna ambavyo KIFO kimeamua kuwachukua bila huruma.
Vijana hawa ambao nimefanya nao kazi kwa vipindi na mazingira tafauti walinifundisha mambo mengi sana.Hata hivyo vifo vyao vimenifundisha Jambo kubwa zaidi.We have limited TIME,Limited Capabilities,Limited Resources,Limited opportunities and we are Limited Editions.
Leo nataka nisisitize zaidi kuhusu mimi na wewe kuwa Limited Editions na namna ambavyo tunaweza kutumia Limits zetu katika kuhakikisha kwamba tunafanya maisha yetu na ya wale wanaotuzunguka kuwa bora zaidi.Wakati naanza kufanya shughuli za biashara nilikuwa kijana mdogo nisiyekuwa na uzoefu ila niliyekuwa na shauku kubwa sana ya mafanikio.
Ninazikumbuka enzi zile ambazo nilifikia kwenye Ofisi za makampuni na kuzungumza na wakurgenzi.Nakumbuka enzi zile nilipkuwa naenda wizarani kuomba miada na waziri viongozi wa taasisi huku nikiamini kabisa kwamba nilikuwa na mawazo ya kipekee na ya kibunifu ambayo yangeweza kubadilisha dunia.Kiukweli hayakuwa mawazo mapya wala ya kipekee. Ila nilikuwa na ujasiri.
Wengi mnaosoma andiko hili mnaweza msiamini ila niliwahi Kupeleka wazo la Mobile Payment(MPESA )kwa meneja mmoja wa Vodacom ambay alikuwa Muhindi SIkuwa najua hata kufanya codind ila niliwaza tu kwamba kama meseji inaweza kutumwa kuonesha muamala umefanyika basi inawezekana.
Nilisha enda hadi TIRDO kueleza wazo la magari y umeme miaka mingi kabla Elon musk hajawa maarufu.Nlshafika Hadi wizara ya teknolojia na sehemu inaitwa costech kabla hawajawa na innovation hubs nikiwa nataka kufanya mrdi wa kuingiza waizara zote mtandaoni ziwe na website,halmashauri zote ziwe na website yaani kuwa na mtandao wa internet wa hudum kwa umma.Kipindi napeleka haya mawazo nilikuwa kijana mdogo,sijui kuandika business plan wala sikuwa na business plan.
Nilijua kuandika Barua kwa kiingereza au kiswahili,niljua kuvaa tai na kupiga viatu rangi.Hakuna hata wazo moja nililofanyia kazi mpaka leo ila nafurahi kwamba yalifanyiwa kazi na sasa mengi ya yale niliyowaza yako tayari.Mimi niliwaza smartphone miaka mingi kabla haijawepo.Baada ya tu ya kuona simu na kuona Computer basi akili yangu iliwaza namna ya kuweza kufanya secreen ya Computer iwe kama ya SIMU yaani iswie ile Chogo bali iwe kama ya simu.na ile circuti ya computer iwe ndogo kama ya simu.au kubwa kiasi.Sikuwa nimewahi kuona laptop(Sidhani kama ilikuwepo sokoni)
Sasa hivi nimekuwa zaidi na tayari failures na changamoto za maisha zimenifundisha uoga.Kabla yakufanya jambo natumia muda mrefu zaidi kuwaza na ninaogopa zaidi kukosea kuliko ninavotamani kufanikiwa au hata kujaribu kufanikiwa.Sipendi hii tabia ila nitabia ambayo wengi.Tunayo.Ujasiri wangu umebaki katika kuandika maandiko JF,huki nikijificha nyuma ya ID na kujaribu kuwatia moyo wengine.Kwa sasa inatosha ila lazima tufnye zaidi.
Sasa baada ya utangulizi huo mrefu nataka nikwambie ukweli Mchungu.Utakufa.Anytime anyhow but UTAKUFA so Make the most of NOW.Anza na ulicho nacho hapo ulipo,usiogope kukosea wala kukosolewa.Wewe sio wa kwanza wala hutakuwa wa Mwisho so Please Start NOW.
Usisubiri kesho au baadaye,Usitafute sababu wala kisingizio,Amka,Anza kuchukua hatua.Anza kubadilisha DUNIA kwa kubadlisha maisha yako.Sikupambi nakwamba ukweli siku moja utajilaumu kwa nini hukuchukua hatua na utaishia kusimulia tu kwamba niliwaza hivi,nilitaka kufanya hivi n.k.Na huenda usipate hata hiyo nafasi ya kusimulia,Utakuwa mavumbini unaliwa na funza.
Ukishakufa huna lako,huna chako,Hata Threads zako JF zinapoa,Hata videmu vyako vitakusahau,masela watakusahau,Mkeo na watoto watakusahau,Ila kama ulifanya mambo yale mambo yatabaki kuwa ni UKUMBUSHO wako duniani hata kama ni madogo.
Anzisha Biashara Mpya ikifa anzisha yingine,ikif anzisha nyingine na nyingine tena.Jifunze vitu vipya.Usiache kuota Ndoto,Usikate tamaa usiogope kujaribu wala usijinenee maneno ya kukata tamaa wala usikatashe tamaa wengine.CHukua HATUA ishi maisha yako kwa viwango vingine.
Mungu akibariki.
Iwapo una maoni zaidi basi tuendelee kuchangia kwenye comment au tuwasiliane kwa email masokotz@yahoo.com Tujadili zaidi
Nakutakia wakati mwema.