Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Nimekuwa najiuliza hadi sasa sijapata majibu na labda kwa kuwa JF kuna wengi baso mengi yanaweza kuwepo pia .Nimeshuhudia magazeti na hasa TBC 1 wakiwa navipindi maalumu juu ya Uchaguzi wa USA hadi wakaonyesha mwekeleo wao wa upendeleo kama kawaida badala ya kuleta habari kwa wananchi .Lakini kubwa ni kwamba TBC1 ilishindwa kabisa kuonyesha na kuelezea matukio ya Tarime kwa undani kwa faida ya watanzania .Kila walipo jaribu kusema lolote la Tarime basi lilikuwa la uongo na kuwapaka matope Waoinzani utadhani wao hawana haki na na TBC1 kama chombo cha kitaifa na kodi yao wapinzani pia inatumika kuiendesha .Mambo ya kutisha yalitokea Tarime lakini TBC walikuwa wa kwanza kupotosha umma .Leo najiuliza ilikuwa vipi habari za USA ziwe na maana sana kuliko habari zetu za Tarime na matumizi mabaya ya kila kitu kuanzia jeshi , mapesa nk ?
Mwenye majibu anisaidie kunielewesha maana mimi naamini Tido Mhando kapoteza mwelekeo kama mwana habari wa Taaluma na kuwa kama Jeshi la polisi la CCM .
Mwenye majibu anisaidie kunielewesha maana mimi naamini Tido Mhando kapoteza mwelekeo kama mwana habari wa Taaluma na kuwa kama Jeshi la polisi la CCM .