bora huyo, kwasababu hana mawazo mengine na wanawake wengine, pamoja na kwamba siku akionjeshwa na mtu wa nje, katu hatoshikika tena, anahama kabisa.
You people have got to understand that, kutulia au kutotulia kwenye ndoa haiji kwa nguvu za mwili. inakuja kwa nguvu ya kushinda dhambi, nguvu ambayo mtu huipata kwa njia ya kuokoka kumpa Bwana Yesu Kristo maisha yake, na kupokea kipawa cha Roho Mt. kitakachomuongoza maisha yake. ukifanya hivyo, hakika mtu akikuletea masuala ya kufanya uzinzi, utatamani kutapika, hutaki kabisa na unachukia dhambi pamoja na kwamba itakuwa inakujaribu mara kwa mara, haitakushinda.
hadi kuuliza swali hilik,watu wanajaribu kufikiri namna watakavyotulia na watu kwenye ndoa wasitoke nje, au wengine wanafikiri labda wale virgin men wanakuwa hawajui. hakuna mtu aliyezaliwa na elimu yoyote ile. kwanza wote mkiwa watu wa Mungu, mtafundishana na mtajikuta mmeenda vizuri tu na maisha yenu mazuri yanaendelea bila shaka. ila kama watu hamjaokoka, hakika nakwambia mtu anaweza akawa virgin man or woman akabambaruka akageuka akawa si kama ulivyomzania. okokeni wajameni.
ukimwi hauishi siku hizi, ni kwasababu kwa nguvu hizi za kawaida watu hawawezi kuushinda uzinzi. pamoja na kwamba ukimwi unaambukizwa na mambo mengine kama blood transfussion etc, lakini ukiwa kwa Mungu jamani utalindwa na yote hayo. hebu fikiri, unakuwa na mume ambaye hajaokoka na unajua wakati wowote anaweza kulala na mwanamke mwingine, au mume mlevi ambaye anaweza kulala na mtu yoyote ulevini, au mke mlevi, asiye na nguvu ya kushinda dhambi....usalama wenu uko wapi?
hapa mwenye akili, atarudi nyumbani atamwambia mkewe au mumewe wabadili maisha, waishi maisha ya kumfuata Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yao. kwasababu bila hivyo nakuambieni, hakuna usalama maishani mwenu.