That the first two years of marriage are the toughest?...
hapana, sikubaliani na hilo.
ugumu unawekwa na wanandoa wenyewe. Kuna wale ambao katika miaka miwili wanakuwa wamejipangia malengo ambayo kama hayajatimizwa utawaona wanaanza kutapa tapa.
malengo yapo mengi, lakini wengi hushindwa kwa haya;
1. presha za wazazi/ndugu/jamii kumtaka mwanamke abebeshwe mimba/awe keshazaa ndani ya muda huo
2. kushindwa kubadilika. Kujirudia kwa tabia za kukera ambazo wanandoa walikuwa nazo kabla ya uchumba, ambapo wengi walidhani baada ya ndoa kungekuwa na mabadiliko.
3. Dhana potofu, ya kwamba baada ya ndoa Mke amechukua role ya mama mzazi badala ya urafiki na mapenzi alokuwa nayo kabla hawajaoana, vile vile Mume kuchukua role ya unyapara na kumnyima mke uhuru wake kiasi cha kumfanyisha mke kuanza rebellion.
4. Reality ya kuamka kitanda kimoja na mtu huyo huyo siku 365 mwaka wa kwanza, 365 nyingine mwaka wa pili...kwa wengine hii ni boredom ya kutosha! nk...