"Maafande naomba kusema jambo unajua nini ama wazazi wangu wangekuwa na uwezo ningefika hadi kidato cha tano na sita hivyo basi ningekuwa daktari. Moja ya ndoto yangu iliyofifia. Na hata nisingekuwa jambazi sugu namna hii"
"Licha ya hayo ninakubali kupokea hukumu kwa uhalifu niliotenda. Mimi ni mkosaji ninastahili kufa"
"na tena ninawashauri wengine Kwamba uhalifu sio jambo lenye mwisho mwema acheni"
Hello wanajf ona sasa hadi nasahau kusalimia. Habari gani wanandugu katika jina la mola mlezi. Binafsi niko vyema kiafya na ni jambo la kushukuru sana. Inshallah.
Nukuu katika aya ya kwanza na ya pili wala si maneno yangu ni maneno ya bwana mmoja aliyewahi kuishi mbali kidogo na upeo wa macho yangu yeye alijiita Daktari Ishola Oyenusi.
Mwandishi mmoja wa kitanzania Yeye aliwahi kuandika kitabu kimoja alichokiita Dunia Uwanja Wa Fujo.
Mtanikumbusha jina lake tafadhali. Huyu mwandishi bwana anatueleza namna ambavyo dunia ni eneo la wababe kadha wa kadha wanafanya fujo hivi mara vile lakini muda unawasaliti. Ndio ni muda! Muda ni msaliti wa maisha ya binadamu. U mbabe, u mnyonge! muda utakusaliti. Mwandishi anatuonesha namna ambavyo Hitla anafanya fujo zake na kuondoka . Anatuonesha pia wengine akina Mussolini na akina Amini wakifanya fujo.Wanapiga, wanaua, wanatesa na kufunga watu lakini nguvu zao zina kikomo!
Kwani wanaishi mpaka leo? Hawapo! Wamekwenda! Muda unawasaliti. Baada ya miaka nendarudi nguvu zao, fujo zao, na Madaraka yao imebaki kuwa stori za udhalilifu na uovu wa fujo zao. Kila mmoja huwakumbuka kwa uovu na kulaani. Pengine!
Nimemkumbuka mzee huyu wa Dunia Uwanja Wa Fujo ili nikulete katika stori ya mbabe mmoja wa Kinaijeria Kama nilivyomtaja aitwa Daktari Ishola Oyenusi.
Wakati vita ya wenyewe kwa wenyewe imekwisha nchini Nigeria katika mwaka 1970, kipindi ambacho Wanaijeria bado wako katika kipindi cha maombolezo na makovu ya uovu na ukatili wa kivita, ghafla kukaibuka janga la ujambazi mkubwa wa kutisha katika jiji la Lagos na pembezoni mwake. Ni ujambazi mkubwa kwasababu kila aliyefanyiwa unyang'anyi aliuawa hata Kama hapakutokea majibizano yoyote ya maneno au silaha.
Jiji lote la Lagos likashikwa na hofu ya kuvamiwa na kupokwa uhai na Mali kwa mtu mmojamoja ama shirika. Hofu iliyoje matukio hayakupoa kuanzia miaka ya 1960 hivi mpaka robo ya kwanza ya 1971? Polisi mjini humo wakawa hawalali kila siku kumtafuta jambazi sugu anayefanya uhalifu ule! Katika harakati zao za kiitelijensia wakapata kugundua kwamba jambazi kuu wa matukio yanayoendelea mjini Lagos kwamba ni Daktari bwana Ishola Oyenusi.
Polisi kuskia jina la Daktari Oyenusi wakafikiri Kwamba Oyenusi ni Daktari wa binadamu lakini baadae ikaja kugundulika kwamba, baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia ada ya kuendelea na high school na awe Daktari kwa mujibu wa ndoto zake, kumbe bwana Oyenusi akajiapiza kuwa Daktari bingwa wa matukio ya uhalifu, akaiba kwenye mabenki, watu binafsi makampuni, na hata viwandani kwa ufundi mkubwa bila kuacha alama za utambulisho wake. Lakini pia akiua kila aliyemkuta kwenye eneo la unyang'anyi wake. Watu na fujo zao bwana huyo ni Oyenusi akitamba uwanjani.
Lakini je ni nani huyu Daktari Oyenusi Kama alivyopenda kujiita? Alizaliwa huko katika jamii ya Oyo nchini Nigeria miaka ya 1940. Maisha yake ya utotoni yanaonesha ni mtoto mwema aliyekulia katika familia ya wazazi wawili lakini njema isiyo na doa lolote katika maswala yahusianayo na uhalifu. Alisoma humo hadi akamaliza elimu ya sekondari lakini kutokana na umaskini akashindwa kuendelea na masomo na hivyo akakimbilia mjini Lagos alipojiingiza kwenye uhalifu wa kutisha.
Huko mjini Lagos mwangani akawa pia na muonekano wa mtu mwema asiye na makuu. Kijana mkimya mwenye upendo kwa kila mtu anayetabasamu kila mara, na hata akapata mchumba mtoto mzuri kabisa mjini humo. Mwanamke ni kishawishi kikubwa cha kuelekea uovu. Wengine husema . Pengine. Mtoto mzuri kama yule bila fedha ataishije nae mjini Lagos? Si ataachwa! Unaambiwa kutokana na upendo wake kwa mlupo huo siku moja katika miaka ya mwanzo wa uhalifu wake aliamua kufanya unyang'anyi katika gari moja ndogo alipopata Naira 400 na Bado akamuua mmiliki na gari akaondoka nayo. Ambapo hata hivyo hizo Naira 400 alimhonga mchumba wake huyu.
Mjini Lagos na pembezoni mwake jina la Dokta Oyenusi lilikuwa la kistar kubwa zaidi na hata likizungumziwa na kila mtu kwa matukio yake magumu.
Waswahili husema kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho wengine husema siku za mwizi ni arobaini. Haya. Ndio kila kitu kina mwisho ule uhalifu wake na Fujo zake kwa miaka karibu mitano watu walishazichoka wananchi, serikali, jeshi, na polisi wote wakaungana , wakashikana Kama zege kumtafuta adui namba moja wa taifa! Doctor Oyenusi akasakwa,akasakwa kila kona, akatamanishwa kwa misafara ya fedha nk Ili anase lakini wapi. Lakini siku moja ya tarehe 27 March 1971 ikawa ni siku ya mwisho wa fujo za Dr Oyenusi kuendelea kutamba mjini Lagos.
Katika kiwanda kimoja , katika eneo liitwalo Wahum polisi walikuwa wametega mtego wa kumtamanisha na kumnasa mwamba bwana Oyenusi. Humo kulikua na fedha taslim Dola 28000 zilizokuwa na afande mmoja kwa jina Police Constable Nwi. Oyenusi na Genge lake wakaingia Kingi kujaribu kupoka fedha hizo kiwandani humo.
Unajua kikatokea wakamvamia Yule polisi chini ya dakika tano wakampora lile begi la fedha halafu wakamuua Constable Nwi na kuondoka na fedha zile. Polisi mawindoni kushtuka Oyenusi hayupo na mwenzao kala shaba. Wakaamua kufukizia Moto. Humo kiwandani wakapigana kwa masaa kadhaa, wenzake na Dr Oyenusi wakakimbia. Dr akajisalimisha mikononi mwa polisi.
Wakati wakimtia pingu alimpiga kikumbo polisi anaemfunga pingu halafu akamwambia. We mpumbavu usingeongea na Mimi kama unavyofanya hapa Kama ningekuwa na silaha. Ningekuua bila ajizi. Polisi Wana maneno magum asee hasa wakimdaka msumbufu.Basi bwana ndio hivyo Dr Oyenusi fujo zake zilikuwa zikielekea Ukingoni. Walimtia pingi wakapakizwa kwenye ndinga haooo kituoni.
Kesi ikatembea na kutembea. Baada ya miezi mitano hivi Doctor Oyenusi alihukumiwa kupigwa risasi hadharani mpaka kufa (death by firing squard) kwa kosa la uhalifu unyang'anyi, na mauaji ya polisi na raia. Cha ajabu humo mahakamani hakuwahi kuonesha kutishika na yaliyomkabili. Oyenusi kwa muda wote huu alionekana mwenye tabasamu pana usoni bila hofu yoyote ya wazi hasa juu ya hatma yake ya kifo.
Baada ya hukumu Doctor Oyenusi akafikiri akaona si vyema kutangulia akhera peke yake hivyo basi akaamua kuwataja marafiki zake sita aambatane nao katika safari hiyo mpya ya akhera.
Hai Ni mabwana
Joseph Asamedike
Ambrose Nwokobia
Ademola Adegbitan
Stephen Ndubwuoku
Philip Ogbolumain
Joel Amamieye.
Siku ya kufa watu Septembe mwaka 1971 watu wapatao 30000 walijitokeza mjini Lagos kushuhudia kifo Cha Dr Oyenusi, Oyenusi na Genge lake walishushwa kutoka katika Van ya jeshi la Nigeria na kuelekezwa katika milingoti ambapo humo hufungwa kwa kamba nzito wahalifu tayari kwa kupigwa risasi. Unaambiwa siku hiyo superstar humo alikuwa Ni Dr Oyenusi tu.
Watu walipiga kelele na miluzi, wakimkejeli na kumdhihaki. Katika Hali isiyozoekeka inasemwa wengine walikwenda na majeneza wakimuonesha na kumwambia utaingia humu baba dakika mbili zijazo! Tofauti na wenzake yeye alikuwa akitabasamu tu mda wote. Baada ya dakika kadhaa za maandalizi juu ya vifo vya Oyenusi na Genge lake Askari watatu waliamriwa kuwapiga risasi vijana hao saba na wakafa kifo kibaya Cha kidhalilishaji.
Kutoka Google.
Nb. Lugha iliyotumika Ni ya kisanaa kukidhi mahitaji ya kilugha ya wasomaji wa Kiswahil.
Ona picha.[emoji116]
View attachment 2468699View attachment 2468700
View attachment 2468709View attachment 2468710View attachment 2468711