Nimekuwa nikipata tatizo la kutopata choo kwa muda mrefu sana naweza kukaa hata wiki nzima bila kupata choo bt nakula vizuri kawaida milo 3 sijui hata hicho chakula kinaenda wapi nimeonana na madaktari wengi kila mmoja akinipa ushauri wake mara kunywa maji mengi nakunywa wapi, mara kula sana matunda nakula matunda katika kila mlo lakini hakuna kitu mara ushibi vizuri bt me kwa kiasi changu nakuwa nimeshiba kabisa pamoja na hayo yote nimetokewa na kitu cha ajabu safari hii nimekaa bila kupata choo hadi jana ilikuwa siku ya nane usiku nikanywa glass ya maziwa baridi sana asubuhi nimepata choo hadi nimeogopa je Doctor inamaana hayo maziwa ndo tiba yangu????