Doctors; Ndugu yangu anableed mwezi wa tatu(3) mfululizo

Sasha7

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2014
Posts
233
Reaction score
56
Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu kwa MWENYEZI MUNGU..kwakunipa PUMZI NA AFYA NJEMA.

Wapenzi, nina Ndugu yangu ana bleed mwezi wa 3 mfululizo na maumivu makali sana ya Tumbo;

UTAMBULISHO WAKE KWA UFUPI;
Umri wake miaka 25,
Ana mtoto wa miaka 4,
Yuko Dar Es Salaam,

HISTORIA YA UGONJWA WAKE;
Alianza kubleed mwezi wa pili mwaka huu 2015..mpaka sasaivi mwezi huu wa 4 bado anableed mfululizo bila damu kukata.

Alipelekwa Muhimbili Hospital wakampima na kusema kua HORMONE ZAKE HAZIJABALANCE NAPIA KIZAZI KIKO WAZI NA BACTERIA WAMEINGIA KWENYE KIZAZI..wakampatia dawa lakini hazikusaidia chochote kile akawa anaendelea kubleed kama kawaida na kuendelea kupata maumivu makali ya tumbo anasema tumbo linamuuma lote mpaka anahisi vichomi..linamuuma juu chini..kushoto..kulia pamoja na chini ya kitovu yaani kwa ufupi pande zote zihusizo tumbo zinamuuma na kulia kila siku.


Alipomaliza dozi pasi na matumaini yoyote yale..wakampeleka kwenye dawa za Asili Ilala Hospital flani nisingependa kuitaja


Napo akapimwa na kusema kua KIZAZI CHAKE KINA FANGUS NA WAMESHAMBULIA MLANGO WA UZAZI..wakampatia dawa za Asili


Sasa ana week ya pili tangu amalize kuzitumia izi dawa..dozi kamili ila anasema kidogo ana nafuu kwa upande wa utokaji wa damu yaani damu imepungua kasi kidogo japo bado inatoka ila maumivu ya tumbo ndio yamezidi


Doctor's msaada wenu muhimu tafadhali..bila ya kumsahau mkuu MziziMkavu..tafadhali usichoke


Na madoctor wengine pitieni hapa mtoe tiba tuweze kumuokoa uyu ndugu yetu..tafadhalini


Mungu awabariki.
 
Last edited by a moderator:
Amepimwa kuthibitisha kama ana fibroids (uvimbe kwenye tumbo la uzazi)?
 
Umejieleza vyema sana ndugu,Kama ni interview tayari umepita,hongera kwa kujua kuwakilisha/kuwasilisha mada
ngoja Doctor's waje,mpe pole jaman MUNGU ATUNUSURU kwa maradhi
 
Amepimwa kuthibitisha kama ana fibroids (uvimbe kwenye tumbo la uzazi)?

hana mkuu majibu ya vipimo ni kama nilivyooleza hapo juu,hana uvimbe kwenye tumbo la UZAZI
 
Amepimwa kuthibitisha kama ana fibroids (uvimbe kwenye tumbo la uzazi)?

sioni kama kuna haja ya kumuuliza maswali mkuu Bingwaman maana mtoa mada Sasha7 keshajieleza vya kutosha na ameeleweka kabisa, katoa maelezo makini ya majibu ya Hospital zote mbili alizopelekwa uyo nduguye,nilitegemea mchango wa namna ya kutatua huo ugonjwa nasio kushindilia maswali ambayo ambayo tayari yameshajibiwa kupitia hayo maelezo yake hapo juu,tuwe tunasoma Post vizuri kabla ya kujibu au kucomment jamani,samahani kama nitakua nimekukwaza lakini penye ukweli pasemwe

Pamoja mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Umejieleza vyema sana ndugu,Kama ni interview tayari umepita,hongera kwa kujua kuwakilisha/kuwasilisha mada
ngoja Doctor's waje,mpe pole jaman MUNGU ATUNUSURU kwa maradhi

ahsante sana mkuu loveleen kwa kujali
 
Last edited by a moderator:

ahsante mkuu kwa maelezo ya ziada Marnah
 
Last edited by a moderator:
wakuu kimya jaman..........!!!!Doctor's njooni
 

Kuna Ukweli Mwingine Hujatupa au Yeye Mwenyewe Hajataka Kukuambia ILA Anaujua. Huyo Ndugu Yako Amevamia Kambi Ya Mwenzake.
 
Bila shaka hapo dr.Mzizi Mkavu atakusaidia.Mi sijui tiba ila nitoe tu angalizo kulingana na mada, Wanawake muwe makini na njia mnazotumia kusafisha huko chini.

matumizi ya vitu vyenye chemicals wengine wanatumia mpaka asali ni hatari, unaua bacteria walinzi wa hizo sehemu na matokea ndio magonjwa ambayo kupona ni shida.
 
Ndugu yako aliwah kutoa mimba miaka ya nyuma na hawakumsafisha vizuri.
 
mpeleke hospitali ya wachina pale sinza mapambano.kuna mtu alikuwa na tatizo kama hilo isipokuwa maumivu tu..wakasema ana uvimbe then walimvomtibia taratibu ukatoweka now kasahau yote.lakini jiandae kwa gharama za matibabu maana wanaweza wakakwambia uanze na dripu 3kila siku na dripu moja 30000 labda.
 
Mtaftieni supplements za vitamin k na vit c...kupunguza haemorrage..anafaa pia kuangaliwa kama ako na cacx(cancer of the cervix)..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…