Wadau wenzangu kwa muda mrefu sasa nimekuwa najiuliza mbona sijawahi kusikia kama kuna ugunduzi wowote uliofanyika wa Tiba au Kinga ya Maradhi fulani hapa nchini kwetu!? Kama yupo Dr aliyegundua basi wanaojua watujuze. Magonjwa kama malaria yamekuwa yanaitesa Africa karne na karne. Nahisi ingekuwa inasumbua huko Ulaya basi Kinga ingeshapatikana. Au ndio ule msemo kwamba Waafrica ni watu wakufundishwa tu cha kufanya lakini hawana akili yakugundua kitu. Nimeshawishika kujiuliza hili baada ya Jamaa yangu kutoka Norway aliyekuja hapa kwetu tz kufanya Research yake/ ni mwanafunzi wa Chuo/Phd. Amekaa miezi 8, alipokuja alipewa tahadhari ya malaria lakini akadai kuwa yeye amepata chanjo huko kwao na hawezi kuugua malaria kwa muda wote atakaokaa tz tena morogoro. Jamaa huyu kashaondoka na kweli hajaugua malaria . Sasa najiuliza nikwanini wenzetu ambao hata magonjwa haya hayapo kwao lakini wanaweza kugundua Tiba au Kinga lakini sisi tunaoteseka na magonjwa haya inakuwa shidaaaaa!!!? Hapa tuwe wa kweli tu na tusije kusingizia Serikali zetu. Tangu Uhuru hadi leo ni zaidi ya miaka 50 sasa. Je ni kipi kipya Doctors/medical wamefanya au kugundua!!?