Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Naona tunarudi 2019 ki style, chupa imebadilishwa tu design lakini kamnyweso ni kalekale.
====
CHADEMA Wilaya ya Dodoma Mjini kimedai kubaini taarifa za wagombea wake kuenguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kupitia mbinu za kuwatafutia kasoro mbalimbali.
Miongoni mwa mbinu hizo ni kuhamisha majina ya wagombea kutoka kata moja na kuyapeleka kata nyingine, hali inayowafanya wagombea hao kukosa sifa kwa kudaiwa kuwa hawajajiandikisha katika maeneo wanayogombea.
Kupata matukio yote kimkoa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bofya hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Akizungumza na wanahabari tarehe 6 Novemba, 2024, Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Dodoma, Stephen Karashan, amesema chama hicho kimebaini mbinu hiyo na kinatoa wito kwa Waziri wa TAMISEMI kutoa tamko la kuzuia mbinu hizo.
“Tangu CHADEMA ianzishwe, hatujawahi kuwa na idadi ya wagombea kama tulionao safari hii, na tunajua tunakwenda kushinda. CCM walisema hatuwezi kushinda mtaa hata mmoja, lakini baada ya kuona tunawazidi nguvu, wameanzisha mpango huu. Juzi, kikosi cha CCM kimezunguka jimbo lote, kikiwa na wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wa vituo, na kuwapa mikakati ya kuwaengua wagombea wetu,” amesema Karashan.
Amedai kuwa majina ya wagombea wao wenye nguvu yamehamishwa kutoka mtaa mmoja kwenda mtaa wa kata nyingine ili kuonekana hawana sifa za kugombea kwa kutokuwepo katika orodha ya waliojiandikisha katika maeneo husika.