LGE2024 Dodoma: CHADEMA yaapa kuwarejesha wagombea walioenguliwa Uchaguzi Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dodoma, Aisha Madoga, ameahidi kupambana kuhakikisha wagombea wa chama hicho walioenguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa wanarejeshwa, akisisitiza kwamba watafanya hivyo bila woga hata kama hawatapendelewa na mamlaka husika.

Madoga ametoa ahadi hiyo mara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Dodoma Novemba 11, 2024. Kabla ya ushindi huo, Madoga alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA) mkoani humo.

Akihutubia wajumbe wa chama mara baada ya ushindi wake, Madoga amepata kura 57 kati ya kura 103 zilizopigwa, akifikia asilimia 54.8 ya kura hizo. Aliwashinda wagombea wenzake, Paul Mashenene, aliyepata kura 20 (asilimia 19.2) na Godfrey Charles, aliyepata kura 26 (asilimia 25).

Amesisitiza kuwa hawatakubali kuendelea kufanyiwa vitendo vya dhuluma na kuenguliwa kwa wagombea wao bila sababu za msingi. Madoga amebainisha kuwa CHADEMA Dodoma imejipanga kuhakikisha inapata ushindi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika mwezi huu.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo vyama vya upinzani vimekuwa vikilalamikia kuenguliwa kwa wagombea wao katika baadhi ya maeneo nchini, hatua wanayodai ni kinyume na misingi ya demokrasia na haki za kisiasa.
 
awarejeshe km nani? Yeye ni tamisemi, Kiki nyingine bwana
 
Good thinking
 
Back
Top Bottom