Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania Anthony Mtaka ameagiza magari ya abiria yanayofanya na kuanzia safari zake mkoani hapo kutosimamisha abiria ikiwa ni hatua ya kupambana na corona.
Mtaka ametoa agizo hilo leo Jumamosi Julai 10, 2021 wakati Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima alipofanya ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kuangalia utayari wa kupambana na ugonjwa huo.
Pia amewaagiza viongozi wa masoko kuhakikisha kuna maji tiririka katika milango ya kuingia masokoni, huku akiwataka wafanyabiashara kuvaa barakoa.
Mtaka ametoa maagizo kwa wote wanaofanya mikutano katika mkoa huo wa Dodoma kuhakikisha wanafuata taratibu za kujilinga ikiwemo kuvaa barakoa, kunawa mikono.
“Maelekezo ya waziri kila mmoja ameyasikia mwisho wa siku anayekukufa, kuugua sio serikali wala hospitali ni wewe chukua tahadhari,” amesema Mtaka.
Akizungumza Dk Gwajima amewataka watanzania kuepuka mikusanyiko isiyolazima ili kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa corona.
“ Tuepuke misongamano isiyo ya lazima na kama ni lazima chukua tahadhari vaa barakoa nawa mikono kwa kutumia maji tiririka tumia vitakasa mikono,”amesema.
Gwajima amewataka kufanya mazoezi pamoja na kuzingatia lishe bora ili kuongeza kinga ya mwili.
Mwananchi