Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jijini la Dodoma ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt. Frederick Sagamiko amesema vurugu zilizoibuka katika kituo cha kupigia kura cha Site 1, mtaa wa Mlimwa, Jijini Dodoma kati ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani humo, Aisha Madoga na wasimamizi wa uchaguzi, ni mpango mahususi wenye nia ovu ya kutia dosari zoezi la upigaji kura.
Dkt. Sagamiko ametoa ufafanuzi huo Jumatano Novemba 27, 2024 ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kusambaa kwa picha mjongeo (Video) kwenye Mitandao ya Kijamii ikionesha vurugu hizo.
Vurugu hizo ziliibuka baada ya mwenyekiti huyo kubaini wapiga kura ambao walielezwa kuwa hawakujiandikisha kwenye daftari la makaazi lakini wakaruhusiwa kupiga kura.