Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Hali ilivyo naona kabisa kuna uwezekano wa kuibuka kwa magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Kipindupindu kutokana na mfumo wa maji taka kuwa wa ovyo katika baadhi ya maeneo yakiwemo ya Mjini.
Kuna chemba ipo mbele ya Ofisi za TAKUKURU na Ofisi za Chama cha Walimu (CWT) zinazotazama na Uwanja wa Jamhuri, imefumuka inamwaga kinyesi na inavyoonekana ni suala la kawaida tu.
Kwa ufupi nikisema Dodoma inanuka na imetapaka uchafu, ninamaanisha, hivi karibuni magonjwa yanasababishwa uchafu kama kipindupindu yataibuka kwa sisi Wananchi tunakula kinyesi.
Moja ya Chemba ipo karibu na bomba na maji safi na mkondo wake pia unaenda kwenye njia za maji safi.
Pia, soma;
√ - DUWASA: Changamoto ya kusambaa kwa majitaka Dodoma, kulikosababishwa na chemba kuziba imetatuliwa