PreGE2025 Dodoma: Kamati ya kudumu ya bunge yapongeza ujenzi wa jengo la wizara ya nishati - Mtumba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
📌Ujenzi wafikia 94%

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekagua ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati katika mji wa Serikali Mtumba na kuipongeza Wizara kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa asilimia 94.
Your browser is not able to display this video.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. David Mathayo amesema hayo tarehe 20 Machi 2025, wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa jengo hilo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma iliyohusisha Menejimenti ya Wizara na baadhi ya watumishi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Tumepita kila mahali katika jengo hilo kazi nzuri na kubwa imefanyika na mandhari ya ndani na ya nje zote zinavutia sana, nawapongeza sana Wizara ya Nishati kwa kazi hii, zaidi kamati inampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana za kutekeleza ujenzi wa majengo mengi na mazuri ya serikali.”

Amesema Mathayo
Amepongeza Viongozi Wakuu na Menejimenti ya Wizara ya Nishati kwa kusimamia vyema ujenzi huo na kuhakikisha fedha za mkandarasi zinalipwa kwa wakati wakati wote.

Aidha,amewasisitiza kukamilisha kazi ndogo zilizosalia ili watumishi waweze kuhamia katika jengo hilo mapema.


Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu, amesema kuwa watumishi wa Wizara ya Nishati wanatarajia kuhamia katika jengo hilo kabla ya mwezi Mei 2025 kwa kuwa kazi kubwa tayari imeshafanyika.

Dkt. Kazungu amesema watumishi wote wakihamia katika jengo kutawazesha watumishi hao kukaa sehemu moja na kufanya kazi zao kwa ufanisi tofauti na ilivyo sasa ambapo watumishi wamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni Kikuyu na Mtumba.
 
JPM forever,kama sio maamuzi magumu haya majengo yangeliishia kwenye matumbo ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…