LGE2024 Dodoma: Katibu wa BAKWATA, Askofu wasema kuna watu hawaitakii mema Tanzania, wanasambaza habari potofu kuhusu uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kuna vitu mpaka aibu unaona wewe! Useless kabisa!

Baadhi ya viongozi wa dini nchini wamesema kuwa wamebaini viashiri vya uwepo wa namba za simu za nje ya nchi zikihamasisha taarifa potofu kwa lengo la kuwagawa Watanzania, huku wakidai kuwa kuna watu ambao hawaitakii mema Tanzania.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Novemba 28, 2024 jijini Dodoma na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assembles Of God, Dkt. Evance Chande pamoja na Katibu wa BAKWATA mkoa wa Dodoma, Hussein Kizungu walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari ambapo wameeleza namna Serikali ilivyosimamia mchakato mzima wa uchaguzi wa serikali za mitaa, uliofanyika jana Novemba 27, 2024.

Aidha, viongozi hao wameeleza kuwa kuna baadhi ya watu watatumiwa kutoa habari za uongo ili kuvuruga amani ya nchi, huku wakiwataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani wakati wakisubiri matokeo ya uchaguzi.
 
kwa mfano kitima na ruwaichi wanatamani sana patokee vurugu humu nchini.

hawahubiri tena habari ya kuwapeleka waamini wao mbinguni kwa Mungu..

wanawachonganisha, wanawachochea na kuwagawa waamini ili wazichape kavu kavu 🐒
 
Wabarikiwe sana viongozi wetu
"Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli huongoza kwenye wema, na wema huongoza kwenye Pepo. Mtu huendelea kusema ukweli mpaka akaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli.

Na jihadharini na uongo, kwani uongo huongoza kwenye uovu, na uovu huongoza kwenye Moto. Mtu huendelea kusema uongo mpaka akaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni mwongo."

(Sahih al-Bukhari, Hadithi ya 6094; Sahih Muslim, Hadithi ya 2607)
 
Hawa ndio matapeli walioamua kusaka pesa kwa kutumia mlango wa dini. Na kwa kauli hiyo, lazima wavute kitita kizuri kutoka CCM.

Hawa ndio walioona karata tatu hailipi, wewe jiite nabii, askofu, shekhe au ustadhi, halafu wakati wote subiria viongozi wa dini waikosoe serikali, kisha wewe unafanya kinyume chake.

Hapa, kwa kauli hii, wana uhakika wa kupata kila mmoja kati ya 50 na 100m. Wanachotakiwa ni kusema wanataka kukarabati au kujenga nyumba ya ibada, halafu wasubirie mjumbe wa Rais ataleta kiasi gani!!!
 
kwa mfano kitima na ruwaichi wanatamani sana patokee vurugu humu nchini.

hawahubiri tena habari ya kuwapeleka waamini wao mbinguni kwa Mungu..

wanawachonganisha, wanawachochea na kuwagawa waamini ili wazichape kavu kavu 🐒
Imefika wakati tupigane tu, damu imwagike, ioete mbegu bora
 
Bakwata wanatutia aibu Waislamu wote tunaonekana wajinga kwa sababu yao,wanaendekeza njaa sana.
Vihela vidogo vidogo wanavyopewa na serikali vinawavua nguo bila wenyewe kujijua! Inasikitisha sana.
 
Wakuu,

Kuna vitu mpaka aibu unaona wewe! Useless kabisa!

Baadhi ya viongozi wa dini nchini wamesema kuwa wamebaini viashiri vya uwepo wa namba za simu za nje ya nchi zikihamasisha taarifa potofu kwa lengo la kuwagawa Watanzania, huku wakidai kuwa kuna watu ambao hawaitakii mema Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Novemba 28, 2024 jijini Dodoma na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assembles Of God, Dkt. Evance Chande pamoja na Katibu wa BAKWATA mkoa wa Dodoma, Hussein Kizungu walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari ambapo wameeleza namna Serikali ilivyosimamia mchakato mzima wa uchaguzi wa serikali za mitaa, uliofanyika jana Novemba 27, 2024.

Aidha, viongozi hao wameeleza kuwa kuna baadhi ya watu watatumiwa kutoa habari za uongo ili kuvuruga amani ya nchi, huku wakiwataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani wakati wakisubiri matokeo ya uchaguzi.
Kama polisi wenyewe wamekiri kumshikilia askari mwenzao aliyeua, hawa vinyamkera wanawaza kwa kutumia kiungo gani
 
Wachumia matumbo wameshaamua akili kuziweka makalioni,, so sad aisee 🚮🚮
 
kwa mfano kitima na ruwaichi wanatamani sana patokee vurugu humu nchini.

hawahubiri tena habari ya kuwapeleka waamini wao mbinguni kwa Mungu..

wanawachonganisha, wanawachochea na kuwagawa waamini ili wazichape kavu kavu 🐒
Ulaanike kwa roho mbaya ya kutojali maisha ya Watanzania wenzako waliouawa kipindi cha uchaguzi.
 
Wakuu,

Kuna vitu mpaka aibu unaona wewe! Useless kabisa!

Baadhi ya viongozi wa dini nchini wamesema kuwa wamebaini viashiri vya uwepo wa namba za simu za nje ya nchi zikihamasisha taarifa potofu kwa lengo la kuwagawa Watanzania, huku wakidai kuwa kuna watu ambao hawaitakii mema Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Novemba 28, 2024 jijini Dodoma na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assembles Of God, Dkt. Evance Chande pamoja na Katibu wa BAKWATA mkoa wa Dodoma, Hussein Kizungu walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari ambapo wameeleza namna Serikali ilivyosimamia mchakato mzima wa uchaguzi wa serikali za mitaa, uliofanyika jana Novemba 27, 2024.

Aidha, viongozi hao wameeleza kuwa kuna baadhi ya watu watatumiwa kutoa habari za uongo ili kuvuruga amani ya nchi, huku wakiwataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani wakati wakisubiri matokeo ya uchaguzi.
Hao sio viongozi wa dini bali ni vibaraka wa CCM na magenge ya wahalifu walio madarakani
 
kwa mfano kitima na ruwaichi wanatamani sana patokee vurugu humu nchini.

hawahubiri tena habari ya kuwapeleka waamini wao mbinguni kwa Mungu..

wanawachonganisha, wanawachochea na kuwagawa waamini ili wazichape kavu kavu 🐒
Huna maarifa. Mwanadamu mwili na roho. Viongozi wa dini lazima wakali maslahi ya roho lakini pia na miili ya waumini. Ndio maana wanajenga hospital na shule . Ujinga pelekeni kwenu.
 
Hao viongozi mbona wana kiherehere hivyo, nani ana mpango wa kuvuruga amani ya nchi eti kwa uchaguzi wa serikali za mitaa? Huo ni unaa na ni uchochezi. Uchaguzi wenyewe ulipooza na kupuuzwa na wananchi wengi hawakwenda kujiandikisha na kupiga kura halafu waseme kuna watu wanataka kuvuruga amani ya nchi, huo ni uchuro. Nchi ina amani na wananchi wake wanaendelea na shughuli zao hawana habari na matokeo ya uchaguzi huo nani aligombea na nani ameshinda, shame on them
 
Tukisema Roma Locuta Causa Finita Est, watu wanatuona wabaya, Wakatoliki Kupitia TEC haiwatetei wakatoliki pekee bali mpaka wavaa Kobazi mnaoisifia Tamisenga, Mwisho wa siku haya ni Maslahi Mapana ya Taifa letu.. Nyinyi wachache mtanufaika lakini vipi Majority yenu?

Ni wakati wa Ndugu zetu katika imani (Waislamu) Kuikataa BAKWATA, haipo kwa ajili ya uislamu bali ipo kwa ajili ya Wanasiasa wa chama kile na Matumbo yao!

Roma Locuta, Causa Finita Est!
 
a
kwa mfano kitima na ruwaichi wanatamani sana patokee vurugu humu nchini.

hawahubiri tena habari ya kuwapeleka waamini wao mbinguni kwa Mungu..

wanawachonganisha, wanawachochea na kuwagawa waamini ili wazichape kavu kavu 🐒
amanu ni muhimu sana ili CCM waendelee kufilisi hii nchi, hai Wajinga sijui askofu wako sahihi. Bila amani hakuna ufisadi, si amani ni muhimu sana
 
shiriki kwenye uchaguzi kwa amani, ukishindwa au ukishinda uchaguzi huo kubali matokeo na kua mustaarabu..

kuchochea chuki zaidi sana utaumia mwenyewe tu 🐒
 
nyie wajinga sana amani ni ni chaka ka kuhadaaa wajinga wa hili Taifa ili wajanja wale na kunywa kwa amani
 
Back
Top Bottom