Dodoma: Mahakama yakabidhi ng’ombe 80 kwa watoto

Dodoma: Mahakama yakabidhi ng’ombe 80 kwa watoto

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
ng%2527ombe.gif
Kundi la Ng'ombe.

KWA UFUPI
Akisoma hukumu hiyo jana Jaji wa mahakama hiyo, Aisha Kwariko, alisema mahakama imejiridhisha kuwa ng’ombe hao 82 ni mali halali ya marehemu Milika Ndudumizi na hivyo walipaswa kugawiwa watoto wake baada ya yeye kufariki.

MAHAKAMA ya Rufaa katika Kanda ya Dodoma, jana iliwapa haki watoto wa marehemu Milika Ndudumizi waliokuwa wamenyang’anywa ng’ombe 82 na mjomba wao na kusisitiza kuwa mifugo hiyo ni mali halali ya watoto hao.

Hata hivyo, mahakama hiyo ilipinga ombi la watoto hao la kutaka kulipwa Sh 20 milioni ,kama gharama za uendeshaji wa kesi hiyo kwa madai kuwa hazikuwa na vielelezo.

Gazeti hili lilikuwa la kwanza kuripoti habari za watoto hao baada ya kupata taarifa kutoka katika Kijiji cha Chipogolo ambako walishakata tamaa kwa madai kuwa mama yao hakuwa mmiliki halali wa mifugo hiyo.

Akisoma hukumu hiyo jana Jaji wa mahakama hiyo, Aisha Kwariko, alisema mahakama imejiridhisha kuwa ng’ombe hao 82 ni mali halali ya marehemu Milika Ndudumizi na hivyo walipaswa kugawiwa watoto wake baada ya yeye kufariki.

Jaji Kwariko alisema kuwa katika kufuatilia kesi hiyo pamoja na ushahidi wa pande zote, ilidhihirika mahakamani hapo kuwa wajomba wa watoto hao hawakuwa na haki ya kuchukua mifugo hiyo. Dodoma: Mahakama yakabidhi ng



 
huwa nafurahi sana mahakama ikitenda haki,haswa kwa wajane na watoto wa marehemu!jaji mungu akubariki ktk kazi zako na maisha yako!
 
Yaani kama wataweza wauze hao ng'ombe haraka sana maana hao wajomb a wataanza ndumba kwa hao ng'ombe watapukutika mmoja baada ya mwingine!kama wanaweza wauze wote wabakize hata 5 tu kama wanapenda kufuga!
 
Back
Top Bottom