Dodoma: Mkutano wa 12 wa Bunge - Kupiga kura ya maoni ya Katiba leo

Dodoma: Mkutano wa 12 wa Bunge - Kupiga kura ya maoni ya Katiba leo

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Historia inatarajia kuandikwa katika Mkutano 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, unaoanza leo, mjini Dodoma wakati litakaposafisha njia kwa Watanzani kwa mara ya kwanza, kupiga kura ya maoni ya Katiba.


MKUTANO wa 12 wa Bunge unaanza mjini Dodoma leo , unaotarajiwa kujadili masuala mbalimbali katika vikao vyake "hasa Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni 2013"
 
...Wauza `unga` kutajwa bungeni:

Khamisi%20Kigwangala.jpg


Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah
Vita dhidi ya usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya kupitia katika viwanja vya ndege nchini iliyoanzishwa na Waziri waUchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, imemvuta Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, ambaye ameahidi kutaja majina wauzaji wa dawa hizo ili kuisadia serikali kuchukuamaamuzi magumu.
Dk. Kigwangala aliliambiaNIPASHEjana kwa njia ya simu kuwa hadi sasa amepokea majina saba ya vinara wanaojihusisha na biashara hiyo na kwamba anaendelea kupokea ushahidi ukiwamo wa picha za watu hao wanawauzia kina nani na wanakaa wapi.
Mbunge huyo amesambaza taarifa kupitia mitandao ya jamii ikiwamo Facebook akiwataka wananchi wenye taarifa za wauzaunga kuwasiliana naye na kumpaushahidi ili awataje bungeni katika mkutano wa 11 wa Bunge unaoanza kesho.
Alisema zoezi la kupokea majina hayo na ushahidi linakwenda vizuri na kwamba mwitikio umekuwa mkubwa kutoka kwa wananchi na kusisitiza kwamba lazima awataje wahusika kwa majina.
Aliongeza kuwa ameandika baruakwa Spika wa Bunge kuomba fursa ya kutoa maelezo bungeni kama mbunge na kwamba atampelekea barua nyingine ili apatiwe nafasi ya kusimama na kutaja majina hayo.
“Mimi siogopi kitu, nikipata ushahidi wa kina nitataja majina ya watu wote waliotajwa na wananchi wanaoniletea ushahidi na katika hili moja ya jina ni la kinara anayetajwa tajwa sana,” alisema Dk. Kigwangallah.
Aliwataka wananchi wenye taarifa zinazojitosheleza kumtumia ili azifanyie kazi kabla ya kuwataja bungeni.
Alisema shinikizo la wanasiasa linaweza kusaidia kuiamsha serikali kupitia Jeshi la Polisi kuanza kupambana na tatizo la dawa za kulevya nchini.
MTAMBO MPYA WAFUNGWA JNIA
Kufuatia malalamiko kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Umegeuzwa uchochoro wa kupitishia dawa hizo kwenda nje,Serikali imefunga mtambo mpya ya kisasa utakazokuwa na uwezo wa kutambua zitakazoingizwa aukupitishwa kutoka ndani na nje nchi.
Dk. Mwakyembe jana alifika katika uwanja huo kukagua mtambo huo wa Rapscan 600 series na kuelezwa na viongozi kuwa umetoka Uingereza na kufungwa kwenye uwanja huo kuanzia wiki iliyopita.
Dk. Mwakyembe akizungumza na NIPASHE katika uwanja huo baadaya kumaliza kukagua mtambo huo, alisema lengo la serikali kuongeza mtambo mwingine ili kukomesha kabisa tatizo la watu wasiokuwa waaminifu kupitishia dawa hizo katika uwanja huo na kuliletea aibu Taifa.
Alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa upande wakenayo imefunga mitambo yake kwa lengo la kukabiliana na dawa hizo na kwamba kutoka na ushirikiano uliopo katika ya vyombo vya usalama ni wazi kuwa itakuwa vigumu kwa mtu kuzipitisha JNIA.
Kwa upande wake Meneja Usalama wa JNIA, Clemence Jingu,alimweleza Dk. Mwakyembe kuwa mtambo huo umefungwa kitaalamu na kwamba hatua iliyobaki ni kufungwa kifaa kijulikanacho kama Soft narc scan.
Jingu alisema katika uwanja huo wameanzisha huduma ya kukagua mizigo ya abiria wanaoingia nchini kutoka nchi mbalimbali nyakati za usiku ambayo awali haikuwapo .
Agosti 16, mwaka huu Dk. Mwakyembe aliwataja maofisa usalama wanne wanaodaiwa kuhusika katika njama za kusafirishwa dawa za kulevya na kuigiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kuwafuka kazi na kufunguliwa mashtaka.
Alichukua hatua hiyo kufuatia kilo 150 za dawa za kulevya zenyethamani ya Sh. bilioni 6.8 kukamatwa Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini zikitokea Tanzania, kupitia JNIA.
Maofisa usalama hao ni Yusufu Daniel Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed Kalungwana.
Pia aliliagiza Jeshi la Polisi kumuondoa mara moja katika uwanja huo, askari wake, Ernest na kumchukulia hatua za kinidhamu kwa kushiriki kwake kwenye njama za kupitisha mabegi sita ya dawa hizo yaliyokamatwa Afrika Kusini.
Pia alisema polisi inapaswa kumsaka Nassoro Said Mangungaaliyevikwepa vyombo vya dola Afrika Kusini na kutoroka na mabegi matatu ya dawa hizo.
Alisema mbeba mizigo katika uwanja huo, Zahoro Mohamed Seleman, anapaswa kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ili kuunganishwa na wenzake kujibu mashtaka ya jinai.
Dk. Mwakyembe pia aliiagiza Idara ya Usalama wa Taifa kuendesha uchunguzi wa kina kwa maofisa wake waliokuwa zamu siku ya tukio, kwa kuchelewa kuwafikisha mbwa wakati mwafaka kukagua mabegi hayo yaliyokuwa na dawaza kulevya.
Takwimu zinaonyesha kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 wamekamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini na kuharibu taswira ya nchi na kusababisha wenzao wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Wiki moja baada ya tukio la wasichana hao kukamatwa, Watanzania wengine wawili walikamatwa Hong Kong wakiwana dawa hizo aina ya cocaine na heroine zenye thamani ya Sh. bilioni 7.6 akiwamo mmoja aliyekamatwa akitokea Dar es Salaam kupitia Dubai hadi Hong Kong.

CHANZO: NIPASHE
 
Matendo hutoa na kuleta maana zaidi ya matangazo kama la bwana Kigwangala
 
...Wauza `unga` kutajwa bungeni:

Khamisi%20Kigwangala.jpg


Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, ambaye ameahidi kutaja majina wauzaji wa dawa .....
CHANZO: NIPASHE

Thubutu.............hata akitaja ataishia kutaja majina feki au mateja!!!!!!!!!!
 
Bunge(22).jpg

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kuanza mjini hapa leo ambapo pamoja na mambo mengine, utajadili miswada sita.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewana Ofisi ya Bunge hapa jana, kikaokitaanza saa 3:00 asubuhi kwa Kipindi cha Maswali na Majibu na baadaye kufuatiwa na Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa mwaka 2013 ambao utajadiliwa hadi kesho Jumatano.
Taarifa hiyo ilisema kesho kutwa Alhamisi, mara baada ya kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu na maswali ya kawaida bungeni, wabunge watajadili Muswada waSheria ya Takwimu wa mwaka 2013 hadi siku inayofuata ya Ijumaa.
Miswada mingine ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Vyama vyaUshirika wa mwaka 2013, Muswada wa Sheria wa Mfuko waAkiba wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu wa mwaka 2013, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 na Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa mwaka 2013.
Mkutano huo pia utajadili Azimio la kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu ushirikiano katika masuala ya kiulinzi.
Aidha, katika mkutano huo, kutakuwa na uzinduzi wa Taarifa ya Maendeleo (Tanzania Human Development Report).
CHANZO: NIPASHE
 
Thubutu.............hata akitaja ataishia kutaja majina feki au mateja!!!!!!!!!!

...labda atakuwanayo yaliyokwisha tajwa na JAMHURIM; kama ifuatavyo:-

"Mapapa wa ¡®unga¡¯ watajwa"

*Kinondoni, Magomeni, Mbezi, Tanga watia fora
*Wamo Wakenya, Wanigeria, waimba taarab Dar
*Wengine wapata dhamana kimizengwe, watoroka
Vita dhidi ya wauzaji na wasafirishaji dawa za kulevya inazidi kupamba moto, na sasaJAMHURIimepata orodha ya watu wengine 245 wanaotajwa kuwa ndiyo ¡®mapapa¡¯ wa biashara hiyo haramu hapa nchini.
Idadi hii ni tofauti na ile iliyochapishwa na gazeti hili katika toleo lililopita. Tofauti na orodha hiyo ya awali, kwenye hii mpya JAMHURI imefanikiwa kupata makazi ya baadhi ya ¡®mapapa¡¯ hao ambao miongoni mwao ni waimba taarab maarufu.
Katika orodha tuliyochapisha hapa chini, baadhi ya mapapa hao ni raia wa kigeni. Majina ya nchi wanazotoka tumeyaonesha kwenye mabano, kama ilivyo kwaWatanzania ambao sehemu wanakotoka pia tumezionesha katika mabano. Majina kadhaa ya ¡®mapapa¡¯ hao hayana majina ya sehemu wanazotoka. Juhudi za kubaini maeneo hayo zinaendelea.
Uchunguzi uliofanywa naJAMHURIkwa wiki kadhaa sasa umefanikiwa kupata orodha ya watuhumiwa hao wakuu ambao asilimia 99 wako rumande wakishikiliwa na vyombo vya dola, huku wengine wakiwa wamefikishwa mahakamani.
Asilimia zaidi ya 90 ya ¡®mapapa¡¯ hao wapo jijini Dar es Salaam, huku maeneo ya Kinondoni, Magomeni na Mbezi yakiongoza kwa kutoa idadi kubwa. Kilo moja ya cocaine inauzwa Sh milioni 50.
Kwenye orodha hii mpya, wamo Watanzania na raia wa mataifa mbalimbali walionaswa kwa nyakati tofauti, wengine wakiwa wamejichimbia kwenye mahekalu katika maeneo ya Mbezi, Oysterbay na Masaki.
Miongoni mwa ¡®mapapa¡¯ hao ni Fredy William Chonde (mkazi wa Magomeni), Kambi Zuberi (Temeke), Abdul Ghan na ShahbazMaliki (Pakistani) waliokamatwa wakiwa na kilo 175 za heroin. Mapapa wawili - Shahbaz na Maliki ambao ni raia wa Pakistani,wametoroka nchini baada ya kupewa dhamana katika mazingira tata.
Papa mwingine, Ally Mirzai Pirbakhish ambaye ni Mpakistani, amekamatwa akiwa na waimba taarabu maarufu ambao wote ni wakazi wa Kinondoni. Waimbaji hao ni Aziz Juma Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman Mtumwa, na Hamidu Kitwana Karimu.
Pia kuna watuhumiwa Ismail Shebe Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader (wote wakazi wa Kinondoni, Dar es Salaam) waliokamatwa wakiwa na kilo 50 za heroin.
Raia wa Afrika Kusini, Jack Vuyo na Anastazia Elizabeth Cloete, wako mbaroni kwa kukutwa na kilo 42 za heroin. Mnigeria aliyetambuliwa kwa jina la Kwako Sarfo amekamatwa akiwana kilo 11.951 za cocaine.
Mapapa wengine ni wakazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Aziz Juma Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman Mtumwa, Hamidu Kitwana Karimu na Mpakistani Ally Mirzai Pirbakhish waliokamatwa wakiwa na kilo 97za cocaine.
Kwenye orodha hiyo wamo Mwanaidi Ramadhan Mfundo ambaye ameolewa na raia wa Kenya, lakini nyumbani kwa wazazi wake ni Mbezi Beach, Dar es Salaam. Wengine ni Sara David Munuo (Kenya), Anthony Karanja (Kenya), Benny Ngare (Kenya), Almas Hamis Said (Kinondoni), Yahaya Haroun Ibrahim (Kinondoni), Aisha Said Kungwi (Mwenge, Dar es Salaam), Rajabu Juma Mzome (Mbezi Luis) na John William Mwakalasya ambayeni mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam.
Aidha, yumo Mtanzania mwenye asili ya Kiasia anayeitwa Rashid Ally Mtopea (mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam) ambaye pamoja na wenzake wawili - Idd Adam Mwaduga (Tanga) na Nurdin Husein (Ilala) wamekamatwa wakiwa na kilo 12 za heroin.
Orodha kamili ya mapapa hao ni:
1: Steven Gwaza (Upanga, Dar es Salaam).
2: Rebecca Wairimu Mwangi (Kenya)
3: Khatibu Bakari Khatibu (Magomeni)
4: Khalid Salimu Maunga (Uingereza)
5: Dhoulkefly Awadhi (Tabata Kimanga, Dar es Salaam)
6: Abdallah Pashua Kipevu (Kinondoni)
7: Diaka Brama Kaba (Guinea)
8: Ndjane Abdubakar (Liberia)
9: Sylivia Kaaya Namirembe (Uganda)
10: Farid Kisuule (Uganda)
11: Robinson Dumba Teise (Uganda)
12: Ismail Mugabi (Uganda)
13: Rashid Salim Mohamed (Uganda)
14: Mini Thabo Hamza (Afrika Kusini)
15: Kwako Sarfo (Nigeria)
16: Hamis Muhamed Mtou (Magomeni)
17: Mustapha Musa (Kinondoni)
18: Amani Saidfadhil Daruwesh (Kinondoni)
19: Afshin Jalal (Kinondoni)
20: Jack Vuyo (Afrika Kusini)
21: Anastazia Elizabeth Cloete (Afrika Kusini)
22: Simon Eugenio Fadu
23: Assad Azziz
24: Ismail Shebe Ismail (Kinondoni)
25: Rashid Salim (Kinondoni)
26: Majed Gholamghader (Kinondoni)
27: Anna Jamaniste Mboya (Kinondoni)
28: Fredy William Chonde (Magomeni)
29: Kambi Zuberi (Temeke)
30: Abdul Ghan (Pakstani)
31: Shahbaz Malik (Pakstani)
32: Livinus Ajana Chime (Nigeria)
33: Chukuwudu Denis Okechukwu(Nigeria)
34: Pailo Ekechkwu (Nigeria)
35: Hycenth Stan (Afrika Kusini)
36: Shoaib Mohamed (Pakistani)
37: Pedro Alfredo Chongo (Kinondoni)
38: Kadiria Said Kimaro (Kawe)
39: Abdallah Rajab Mwalimu (Magomeni Kagera)
40: Mwiteka Godfrey Mwandemele (Kinondoni)
41: Abbas Kondo Gede (Kinondoni)
42: Mwanaidi Ramadhan Mfundo (Kenya)
43: Sara David Munuo (Kenya)
44: Anthony Karanja (Kenya)
45: Benny Ngare (Kenya)
46: Almas Hamis Said (Kinondoni)
47: Yahaya Haroun Ibrahm (Kinondoni)
48: Aisha Said Kungwi (Mwenge)
49: Rajabu Juma Mzome (Mbezi Luis)
50: John William Mwakalasya (Temeke)
51: Ally Mirzai Pirbakhish (Pakstani)
52: Aziz Juma Kizingiti (Kinondoni)
53: Said Mashaka Mrisho (Kinondoni)
54: Abdulahman Mtumwa (Kinondoni)
55: Hamidu Kitwana Karimu (Kinondoni)
56: Ramadhan Athuman (Tanga)
57: Rashid Mohamed (Tanga)
58: Ally Mohamed Kichaa (Tanga)
59: Issa Abdurahman (Tanga)
60: Rashid Ally Mtopea (Magomeni)
61: Idd Adam Mwaduga (Tanga)
62: Nurdin Hussein (Ilala)
63: John Adam Igwenma (Nigeria)
64: Ismail Adam au Athuman Yamvi a.k.a Rasta (Afrika Kusini)
65: Ahmed Said Mohamed (Temeke)
66: Morine Amatus Liyumba (Kinondoni)
67: Upendo Mohamed Cheusi
68: Abdallah Omary Salum
69: Salama Mashaka
70: Ekene Paul Ndejiobi (Nigeria)
71: Hamis Hemed Issa
72: Lwaretta Chioma Ani (Nigeria)
73: Cosmas Chukwumezie (Nigeria)
74: Ifeanyi Malven Kalu Oko (Nigeria)
75: Sunday Valentine Ugwu (Nigeria)
76: Allan Duller (Ireland)
77: Alberto Mendes (Ghana)
78: Joseph Chukwumeka Nwabunwanne (Nigeria)
79: Kwaku Safo Brobbery (Ghana)
80: Princewill Ejike (Nigeria)
81: Mary Mvula (Zambia)
82: Waziri Shaban Mizongi (Dar es Salam)
83: Santos Joseph Mpondela (Dar es Salaam)
84: Kelven Kelven Mwanzen (Dar es Salaam)
85: Emmanuel Adom (Ghana)
86: Asha Omary Ramadhan
87: Mariam Mohamed Said (Kinondoni)
88: Abdullatif Fundikira
89: Marceline Koivogui (Guinea)
90: Edwin Cheleh Swen (Liberia)
91: Benjamin Obioma Onourah (Nigeria)
92: Sofia Seif Kingazi (Kinondoni)
93: Josephine Mumbi Waithera (Kenya)
94: Idd Juma Mfaume (Dar es Salaam)
95: Amina Kasim Ramadhan(Kinondoni)
96: Vivian Edigin (Nigeria)
97: Hadja Tambwe (Kinondoni)
98: Sasha Farhan Mnyeke (Kinondoni)
99: Mychel Andriand Takahindangeng (Indonesia)
100: Kristina Biskasevskaja (Luthenia)
101: Stephen Basil Ojiofor 28 (Nigeria)
102: Judith Marko Kusekwa (Tabata)
103: Khamis Said Bakari (Kinondoni)
104: Tabia Omary au Neema Omary (Kinondoni)
105: Hamisi Abdalah
106: Haji Salum Mintanga
107: Mohamed Ally
108: Pendo Stanley Msaki
109: Ramadhani shabani
110: Nickson Jackson
111: Mussa Lazaro
112: Joseph Msami au Kombe
113: Tile Godfrey
114: Upendo Samweli
115: Joseph Loiruku Manina
116: Karim Benajira na Mwanaisha Ally
117: Prosper Charles
118: Fraiaza Benjamin au Babu
119: Richard Godfrey au Loisor
120: Iddi Rajabu
121: Ally Mohamed na Juma Salum
122: Sophia Rashid na Latifa Ally
123: Khalifa Said
124: Estomi Joel au Sangi
125: Abdala Hamza au Haule
126: Haji Bakari
127: Jasmine Tesha
128: Evance Sebastian
129: Goodluck Anael Mtui
130: Estomih Peter Msuya
131: Laitness Kiando
132: Juma Said
133: John Alex
134: Said Maruku
135: Mohamed Rajabu
136: Simon Sebastian
137: Joyce Francis
138: Hussein Hassan
139: Simon John
140: George Matowo
141: Fred Maloli
142: Rashid Abdallah au Buriburi
143: Paulo Baton,
144: Kashinje Seleli,
145: Sheha Kapaya
146: Moshi Joseph
147: Said Mshana
148: Elias Matelema
149: Pascal John
150: Ramadhan Mohamedi
151: James Samwel
152: Adamu Glehamu au Muhomba
Mrisho Simba
153: Juma Kassim au Malila
154: Sadal Jamal
155: Deogratius Ndasi
156: Saada Ally Kilongo
157: Obiesie Gabriel Chibueze (Nigeria)
158: Kennedy Elias Shayo
159: Athumani Musa
160: Abdallah Hamza au Haule, Andrew
161: Mkandilo
162: Abass Abubakar Swai
163: Haji Ibrahim
164: Mwenye gari T 526 BWK
165: Venance Sebastian
166: Hussein Mohamed
167: Bahati Joseph
168: Sadiki Diwani Mhindi
169: Shabani Selemani
170: Yusuph Alawi
171: Kurwa Mbwana
172: Amina Ahmed
173: Joachim Ikechu (Nigeria)
174: Said Ally
175: Ally Juma
176: Miraji Salim
177: Hassan Amri
178: Liviston Bathoromeo,
179: CPL Edward
180: PC George
181: Levila Mollel
182: Levava Londondawa,
183: Saiburu Khuresoi Lukumay,
184: Laskari Lenye Mollel,
185: Kunini Lenye Mollel
186: Saning¡¯o Keuya Mollel
187: Livingstone Matholomeo Urasa
188: Mikidadi Hussein au Athuman
189: Masesa au Habaiba Andrew Joseph
190: Allen Habib
191: Harrison Chigozia Ubah (Nigeria)
192: Njani Hassan Kapaya
193: Adamu Rashid Jalal
194: Idd Hassan Chomu
195: Karim Renajira
196: Khadija Hussein Lukanga
197: Fraizer Benjamin au Babu
198: Bahati Joseph
199: Abdul Mohamed
200: Raheli Yona
201: Simon John
202: Juma Ramadhani
203: Zephania Laizer
204: Adoloph Thobias Mushi
205: Mrisho Simba
206: Danie Kumuo
207: Ally Ramadhani
208: Anna Samweli
209: Felista Kalembo
210: Hussein Hassan
211: Mussa Bwana Mrisho
212: Hakuna
213: Iddi Jumanne
214: Hussein Rashid
215: Joyce Francis
216: Musa Murigo
217: Mohamed Said
218: Oddoi Onesmo
219: Benard Reginald
220: Felista William
221: Allykad Alfonce
222: Selemani Rashid
223: Adam Gleham Mhomba
224: Pius Laurence
225: Jasmin Tesha
226: Juma Ramadhani
227: Soloka Ally na Wenzake wawili
228: Madege Pakasi
229: Joseph Polikapi
230: Emmanuel Absolom
231: Ally Ramadhani
232: Petro Simon
233: Said Mohamed Mollel
234: Raphael John
235: Abdul Ayubu
236: Samweli Loshilari
237: William Matei
238: James Wilison
239: Godfrey Fanuel
240: Rebeka Abdallah
241: Rukia Ally
242: John James
243: Agustino Julius
244: Joseph Lucas
245: Praygod Maliki.
By: © 2013JamhuriMedia

...my take: Labda atatuletea orodha mapapa wakubwa' wasiyokuwemo kwenye hii orodha.
 
0„8 2013 MCL

Bunge lisijadili miswada hii kwa kulipua:

bunge.jpg

Wabunge wakiendelea na shughuli za Bunge mjini Dodoma.

"Kulingana na ratiba hiyo, Bungepamoja na mambo mengine litajadili na kupitisha miswada sita ambayo wachunguzi wa masuala ya Bunge wanasema itakuwa vigumu kuijadili kwa kina na umakini katika muda huo mfupi uliopangwa."

Bunge linaanza mkutano wake wa 12 mjini Dodoma leo likiwa linakabiliwa na ratiba nzito yenyeshughuli zilizopangwa kuchukua wiki mbili.
Kulingana na ratiba hiyo, Bunge pamoja na mambo mengine litajadili na kupitisha miswada sita ambayo wachunguzi wa masuala ya Bunge wanasema itakuwa vigumu kuijadili kwa kina na umakini katika muda huomfupi uliopangwa.
Wasiwasi huo pengine unatokana na ukweli kwamba katika miaka ya hivi karibuni Bunge limekuwa na historia ya kupitisha miswada ya sheria kwamtindo wa kulipua.
Wabunge wengi wamekuwa hawako makini katika kuisoma na kuijadili kabla ya kuipitisha. Upo ushahidi usiopingika kwamba miswada mingi, hasa yenye maudhui ya kisiasa imekuwa ikipitishwa kiitikadi tu pasipo kupima masilahi mapana kwa taifa. Mfano ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2012 uliopitishwa kishabiki Bungeni na baadaye kurudishwa huko kurekebisha upungufu uliojitokeza.
Ni jambo la kushangaza kwambamiswada isiyo na mwelekeo wa kisiasa pia imekuwa haisomwi wala kujadiliwa kwa umakini na wabunge. Miswada hiyo hupitishwa tu na idadi ndogo ya wabunge waliohudhuria na mijadala yake hukosa hamasa, mvuto na umakini kutokana na kutogusa masilahi ya wabunge na vyama vyao moja kwa moja.
Matokeo yake ni kwamba wananchi wanapopiga kelele kupinga kupitishwa kwa sheria husika ndipo miswada ya kurekebisha sheria hizo hurudishwa Bungeni, kama tulivyoshuhudia wakati Serikali iliporudisha Bungeni Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2012, baada ya wananchi kupinga kuondolewa kwa fao la kujitoa.
Tumesema yote hayo ili kutoa tahadhari kwa Bunge kutoendeleza utamaduni huo katika Mkutano wa 12 unaoanza leo. Wananchi wanataka kuona Bunge likiwa makini katika kusoma na kujadili miswada hiyosita kabla ya kuipitisha au kuirudisha serikalini kama itakuwa na kasoro zisizoweza kurekebika katika muda huo wa wiki mbili. Bunge lazima lisome alama za nyakati kwamba wakatiwa kujadili na kupitisha miswadakwa mazoea umekwisha na kwamba wananchi sasa wanataka Bunge nalo liwajibike kwa kujiwekea utaratibu wa kupata matokeo makubwa kwa haraka.
Miswada itakayojadiliwa ni ya: Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji; Sheria ya Takwimu; Sheria ya Vyama vya Ushirika; Sheria ya Mfuko wa Akiba wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu; Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba; na Sheria yaKura ya Maoni. Kama tulivyodokeza hapo juu, mingi ya miswada hiyo ni nyeti.
Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni na wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kwa mfano ni miswada nyeti inayohitaji wabunge wawe makini na watangulize masilahi ya taifa katika kuisoma na kijadili kabla ya kuipitisha.
Sisi tunalitakia Bunge heri na fanaka katika Mkutano wake wa 12. Hata hivyo, tunadhani uongozi wa Bunge ungepunguzabaadhi ya shughuli zilizopangwa ili kutoa muda wa kutosha kwa wabunge kuijadili miswada nyetiya Kura ya Maoni na Marekebisho ya Katiba.
Ili kufanikisha hilo, tunapendekeza Bunge litengue kanuni husika ili kipindi cha maswali na majibu kifupishwe, ikiwa ni pamoja na kuahirisha uzinduzi wa Taarifa ya Maendeleoya Nchi na kufuta Semina ya wabunge kuhusu Mradi wa Vijiji vya Milenia.

By: 0„8 2013 MCL
 
Back
Top Bottom