Dodoma: Peter Mwakiposile amuua mkewe kisa Kikoba

Dodoma: Peter Mwakiposile amuua mkewe kisa Kikoba

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Peter Mwakiposile kwa tuhuma za kumuua mkewe Aisha Ramadhani mkazi wa Chidachi kwa kumpiga hadi kufariki, kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani akitafuta fedha za rejesho la kikundi cha kikoba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ACP Martin Otieno ameeleza kuwa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wakati akisubiri taratibu za kufikishwa Mahakamani huku mwili wa marehemu Aisha Ramadhani ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa taratibu za mazishi.

20220907_121310.jpg
 
Duh mume anaacha ela ya nyama anakuta mchicha, sababu unaambiwa hakua na hela ya mchezo! Tho haijustify kuondoa uhai wa mtu ila kiufupi hali ya maisha mtaani ni mbaya sana ... counseling inahitajika watu waweze kucoup na hii hali.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Peter Mwakiposile kwa tuhuma za kumuua mkewe Aisha Ramadhani mkazi wa Chidachi kwa kumpiga hadi kufariki, kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani akitafuta fedha za rejesho la kikundi cha kikoba...
Serikali iingilie kati hivi VICOBA vipigwe marukufu this is too much now watu wataendelea kufa tu
 
Mwanaume anakuoa hakuna cha nguo wala mafuta ya kupaka... sana sana ukimpata ambaye kidoooooogo mwenye afadhali atakulipia ada tu za watoto na chakula cha home mengine utajiju.

Sasa huyu mwanamke jobless na mwenye mahitaji yake muhimu ataishije bila vikundi vya kujiwekea akiba na kukopa?
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Peter Mwakiposile kwa tuhuma za kumuua mkewe Aisha Ramadhani mkazi wa Chidachi kwa kumpiga hadi kufariki, kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani akitafuta fedha za rejesho la kikundi cha kikoba...
Namuonea wivu katangulia ameepukana na tozo. Atakocho miss ni mabasi mapya 60 esta.
 
Mwanaume anakuoa hakuna cha nguo wala mafuta ya kupaka... sana sana ukimpata ambaye kidoooooogo mwenye afadhali atakulipia ada tu za watoto na chakula cha home mengine utajiju. Sasa huyu mwanamke jobless na mwenye mahitaji yake muhimu ataishije bila vikundi vya kujiwekea akiba na kukopa?????
Yaan umeseeeema? Emu rudia mama 50/50 hatujakusikia Ongeza sauti kidogo wale wa kule nyuma hawajasikia vizuri....
 
Back
Top Bottom