Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, leo tarehe 18 Oktoba, 2024 amempokea rasmi, Mkandarasi Kampuni ya DERM Group (T) Ltd; Kampuni ya ndani, iliyoshinda kandarasi ya Mradi wa Kusambaza Umeme kwenye vitongoji 150 vya majimbo kumi (10) ya mkoa wa Dodoma, Mradi unaotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka miwili, kuanzia sasa.
Katika hafla hiyo; Mhe. Rosemary Senyamule ameishukuru Serikali kwa kutoa Shilingi Bilioni 18.2 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Kusambaza Umeme kwenye Vitongoji (HAMLET PROJECT II) katika vitongoji 150 vya mkoa wa Dodoma ambapo Wateja wa awali wanaotarajiwa kuunganishwa na huduma ya umeme, watakuwa 4,950.
“Mkoa wa Dodoma una jumla ya vijiji 580 ambapo kati ya hivyo vijiji 560 vimepata huduma ya umeme kupitia Miradi ya awali ikiwemo REA Awamu ya tatu Mzunguko wa Kwanza, REA Awamu ya Pili na REA Awamu ya Kwanza.
Soma Pia:
Kwa upande wa Viongozi wa REA, wakiongozwa na Msimamizi wa Miradi Kanda ya Kati, Mhandisi, Aneth Malingumu amemwambia Mkuu wa mkoa wa huyo kuwa, vitongoji 1,631 kati ya vitongoji 2,892 sawa na asilimia 56 vimekwisha kupatiwa umeme kupitia Miradi mbalimbali ya Wakala (REA) na TANESCO. Sambamba na hivyo, vitongoji 150 vitapatiwa umeme kupitia Mradi wa vitongoji vya majimbo kwenye mwaka huu wa fedha Fedha wa 2024/25. Aidha, vitongoji 1,111 vilivyosalia vitaendelea kupatiwa umeme kwa awamu nyingine na kulingana na upatikanaji wa fedha.

- Mhandisi Deogratius: Tsh. Bilioni 16.7 kusambaza umeme Vitongoji 150, kunufaisha Kaya 4,950
- Morogoro: RC Malima awasisitiza Wananchi kutunza miundombinu baada ya REA kuanza kusambaza umeme katika Vitongoji 166