OR TAMISEMI
Ministry
- Jul 3, 2024
- 20
- 93
Akifungua mafunzo hayo kuhusu utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa wawezeshaji wa Kitaifa mapema leo Julai, 9, 2024 jijini Dodoma, Ndunguru amewataka wawezeshaji hao kwenda kuwezesha mafunzo watakayoyapata ili malengo yake yaweze kutimia kwani Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza Mikopo irudishwe na isimamiwe kikamilifu.
“Ninafahamu kuwa uandaaji wa Kanuni, Mwongozo, vitini vya mafunzo pamoja na maboresho ya Mfumo wa Kielektroniki wa utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi umekamilika, niwapongeze wote mlioshiriki kukamilisha nyenzo zitakazowezesha utoaji wa mafunzo kwa wasimamizi na vikundi kabla ya kuanza kutoa mikopo kama ilivyoelekezwa na Serikali,” alisema Katibu Mkuu Ndunguru.