Mwananchi wa Kawaida
Member
- Feb 9, 2012
- 65
- 15
Katika Hali inayoonyesha kuzidi kukomaa kwa rushwa Tanzania na hasa ndani ya jeshi la polisi askari wa usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma wanaonyesha waziwazi kusuka mipango ya kula hela za madereva wanapowakamata na makosa babarani bila kuwafikisha vituoni.
Tabia hii inaonekana zaidi kwa Polisi wanaosimama barabara ya Dodoma-Singida ambako rushwa imekuwa ikiombwa waziwazi kuanzia Tsh 5000 mpaka Tsh 20000 kwa makosa anayokutwa nayo dereva bila kujali idadi yake.Nasema wanasuka mipango kwa sababu mara nyingi wanajificha na tochi kwenye miti mirefu na penye msongamano wa watu au magari mabovu na wanachagua magari ya kumulika wakijua lazima wahusika watakuwa na cha kuwapa bila kufika kituoni.Sikatai kwamba wanatimiza majukumu yao ila kuna mambo yanatia shaka katika utekelezaji wa majukumu haya

- Kwanza ni utaratibu wa kuangalia speed za magari ambapo ikizidi 50km/h unatakiwa kulipa faini ya elfu 30,tatizo hapa ni kwamba barabara husika haina kibao hata kimoja kuanzia Round about mpaka $ 4 Ways kinachoelekeza mwendo na hii ni ngumu sana kwa watu wanaotoka maeneo tofauti kujua kikomo cha mwendo barabara husika
- Pili.Utaratibu wa askari kusimama unafanyika mara nyingi mwisho wa mwezi,siku za sikukuu na mwezi kama huu ambao watu wengi wanapeleka watoto mashuleni ikimaanisha ni wakati wanapohitaji pesa zaidi
- Tatu.Hawatembei na dicuments zozote za sheria barabarani zinazoelezea haki na wajibu wa dereva kwani sheria za barabarani zainabadilika mara kwa mara zaidi madereva wanaadhibiwa kwa sheria wasizozijua
- Nne.Mara nyingi wnachagua magari ya kukamata(kama nilivyosema awali),hawakamati magari ya serikali,magari yaliyochakaa na magari ya masafa marefu hata kama yako mwendo mkali sana na wakikukamata wanatoa vitisho vingi vikiwemo kukupeleka kuacha gari kituoni mpaka uligomboe,kwenda jela,kunyang'anywa gari,kulipa faini kubwa zaidi ili dereva atishike na kutoa hela anayoambiwa kiurahisi bila kubisha