Dodoma: Waomba wauzike mwili wa rafiki yao anayedaiwa kujinyonga kituo cha polisi

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Kwa nini wasipewe mwili wa rafiki yao kama ndugu hawajatokea?

=======

Siku 12 zimepita huku mwili wa fundi ujenzi Gaston Moshi (25) ukiwa mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kutokana na ndugu zake kutojitokeza, huku marafiki wakiiomba hospitali kuwakabidhi wakauzike.

Kifo cha Moshi kimekuwa na utata, kwani inadaiwa alijinyonga katika kituo cha Polisi cha Bonanza jijini Dodoma.

Hata hivyo, kumekuwa na sintofahamu jinsi kifo chake kilivyotokea huku baadhi wakidai walikuwa wakigombania mwanamke na askari wa kituo cha Bonanza ambaye alienda kumkamata katika eneo lake la kazi.

Akizungumza na Mwananchi kwa niaba ya marafiki hao ambaye hakutaja jina litajwe gazetini alisema Moshi wameishi naye kwa upendo, hivyo kuzikwa na jiji si jambo zuri kwao na hata kwa Mungu.

Alisema wamefanya jitihada za kuwatafuta ndugu zake, lakini imeshindikana na hospitali inasubiri zifike siku 14 ili marehemu azikwe na Jiji la Dodoma.

“Katika maisha kuna kuzaliwa, kuoa na kufa, tunaomba tumsitiri ndugu yetu licha ya utata wote. Manispaa huwa wanafukia hawaziki, sisi tupo tunaomba tupewe mwili tukazike,”alisema rafiki huyo.

Hospitali yasubiri ndugu

Akizungumza na Mwananchi, ofisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa ya General, Tumaini Mbwilo alisema Septemba 7, saa 4.21 usiku waliupokea mwili wa Gaston Richard kutoka Mtaa wa Chamwino.

Alisema taarifa ya daktari inaonyesha marehemu alikuwa amejinyonga na mwili wake umeendelea kuwepo katika hospitali hiyo kutokana na ndugu zake kutojitokeza.

“Bado tunaendelea kuwasubiria ndugu hakuna aliyekuja na siku 14 zikifika Jiji watakuja kuuzika huo mwili,” alisema.

Ilivyokuwa

Fundi mwenzake, Abdul Khamis alisema Jumatano ya Septemba 7, mwaka huu afande ajulikanaye kwa jina la moja la Samweli alifika katika eneo lao la kazi akiwa na gari lenye namba za usajili T497 DMS na kumuulizia marehemu.

Alisema wao wanafanya kazi katika kiwanda cha mabati cha Ando kilichopo Zuzu Jijini hapa na shughuli yao ni kufyatua matofali.

Khamis alisema askari huyo alipofika amlitaka kuingia moja kwa moja na gari hiyo, lakini mlinzi aliyekuwepo alimkataza akimtaka aandikishe kwanza jina.

Alisema alipofika alimkamata na kumfunga pingu na kuondoka naye bila ya wao kujua wanaelekea wapi.

“Tulipomuuliza yule askari shida ni nini, alisema kuna dada amekwenda kituoni na kudai Gaston amempokonya simu yake, hatukuhoji sana tukajua ataenda na yatakwisha,”alisema.

Khamis alisema baada ya kukamatwa Gaston hakuonekana kazini kwa siku tatu, hivyo ilivyofika Jumapili ikabidi waanze kumtafuta.

“Tulijua yupo kituo cha polisi cha Bonanza, baada ya kumpigia simu afande Samweli kwa sababu siku ile aliacha namba za simu getini alipofika kumkamata marehemu,” alisema.

Khamis alisema walikwenda mpaka katika kituo cha polisi Bonanza, lakini hawakumkuta na walipomuulizia waliambiwa wasubiri watapewa majibu.

“Ilibidi tumpigie simu tena afande Samweli na alifika kituoni alitueleza kuwa marehemu alijinyonga kwa kutumia shati kituoni hapo na mwili wake wameupeleka mochwari katika hospitali ya Rufaa ya General,” alisema.

Alisema walipokwenda hopitalini hapo walikuta ni kweli mwili wa Gaston upo na maelezo waliyopewa ni kwamba utazikwa leo.

“Simu zake (marehemu) wanazo polisi sisi hatuwajui ndugu zake na namba za ndugu zake zipo katika ile simu ambayo ipo polisi. Tunaumia kusikia mwili wake unataka kuzikwa na hospitali,” alisema.

Akiendelea kusimulia Khamis alisema wakati akikamatwa marehemu alikuwa akidai kuwa askari huyo amekuwa na uhusiano na mpenzi wake.

“Hata hiyo simu ambayo inadaiwa alimnyang’anya alikuwa ameinunua yeye mwenyewe,” alisema fundi huyo.

Alisema maswali wanayojuliza wao ni kwanini asitoa taarifa katika kiwanda kwamba Gaston alijinyonga mpaka walipofika wao kuulizia.
 
Ingiekuwa nchi nyingine,huyo askari samweli angekuwa mtuhumiwa namba moja.

Ila hapa police wenyewe wanalindana.
 
Polisi wa bongo wanatenganishwa na uzi mwembamba sana na genge la uhalifu. Tangu awamu ya 6 iingie madarakani, naona wamekuja na maigizo ya watu kujinyonga kwa kutumia madekio, na bla bla nyingine.

Siku hizi wamepunguza zile porojo zao za mtuhimiwa kuruka kwenye gari akiwa na pingu, mtuhumiwa kujaribu kukimbia baada ya kwenda kuwaonesha wahalifu wenzake, nk.
 
Ila nanyi wanaume muwege mnaangalia wanawake wa kuwa nao.mtaisha
Wengine sio binadamu.simu umnunulie mwenyewe,kesho ugundue ana mwanaume mwingine ukiamua kuchukua simu yako unaitiwa mwizi..
 
[emoji2367][emoji2367][emoji2367][emoji527]police bhana wanakuwaga na udhaifu na mashaka kuliko hata raiya wenyewe.....asa unauwa mtu kisa mapenzi wewe hujioni mjinga utamwambia nini huyo mwanamke mana anajua kila kitu ...
 
Kama hali ndiyo hii, Jeshi la Polisi linapaswa kutolea Ufafanuzi wa kina juu ya hiki Kifo.

Haiwezekani ujue pa kumkamata mtu, halafu ajinyongee kwako ushindwe kurudi ulipomtoa kuwajulisha kuwa mtu wao amefariki..

Ubinadamu unazidi kupotea kwenye Jamii.
 
Inasikitisha sana.
 
Katika watu ninao wakubali humu jf ww ni mmojawapo, yaan unatumia busar sana kwenye comments zako. Nakufuatilia sana hata kwenye michezo kule, you are really a great thinker.
 
Katika watu ninao wakubali humu jf ww ni mmojawapo, yaan unatumia busar sana kwenye comments zako. Nakufuatilia sana hata kwenye michezo kule, you are really a great thinker.
Kweli mkuu. Japokuwa huwa anapaniki Chadema ikishambuliwa.
 
Katika watu ninao wakubali humu jf ww ni mmojawapo, yaan unatumia busar sana kwenye comments zako. Nakufuatilia sana hata kwenye michezo kule, you are really a great thinker.
 
Nitazidi kusema Kila siku kuwa Hawa wapuuzi kuwaita Jeshi la polisi ni kukosea Sana neno Jeshi. Hili si Jeshi Bali Genge la polisi.

Nirudi kwenye Uzi, how is it possible mtu kujinyonga akiwa polisi? Wanatuona wabongo ni wepesi Kama akili zao.

Na bila shaka the case is over, then Kuna watu wanajiita ma detective[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] detective bongo... Chanzo Cha kifo kichunguzwe.

Polisi Tanzania ni Genge la wahuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…