peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo...
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo...
Ili tuione demokrasiaTunatarajia ccm ita print fomu nyingi kadri iwezekanavyo kwa ajili ya wagombea Rais 2025.
Hata Wewe ukichukua fomu utamshinda ndani ya chama chakeIli tuione demokrasia
Kwa hiyo campaign zimeanza?😃😃Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo...
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, watanzania hawajaelewa kilichompata mpendwa wetu JPM , sasa kampeni uliyoianza ni biashara haramu. Dr Bashiru Ally Kakurwa Ana ujumbe kwa watanzania atautoa 2024Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo...
Hii ndio kazi anayoiweza, nyie mkampeleka eti ahamasishe Stars....maweeeeWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mawaziri na naibu mawaziri.
Majaliwa amewataka mawaziri na naibu wao kuwa wasemaji wakubwa wa mafanikio ya Serikali ili itakapofika 2025, Samia Suluhu Hassan (Rais) apite na kusema kidogo tu.
"Wambieni wananchi kuhusu mazuri yanayofanywa na Serikali hii, tambueni msimamo na mtazamo wa Rais ili mkawe wasemaje zaidi yeye akija awe na maneno machache ya kueleza," amesema.
Waziri Mkuu amewataka mawaziri na naibu wao kufanya kazi kwa mashirikiano na kuheshimu kauli za viongozi wakuu kwani siyo kila agizo lazima waandikiwe barua ndipo watekeleze.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuwa mfano kwa mienendo yao wakianzia na mavazi, kauli na kutojiinga katika mambo yatakayowafanya wajadiliwe.