Don Gorgon
Member
- Nov 21, 2024
- 35
- 68
Wenyeviti 36 na wajumbe wa serikali ya mitaa 180 katika Halmashauri ya Mji Kondoa Mkoani Dodoma wameapishwa tayari kuanza kutekeleza majukumu yao katika serikali za mitaa.
Akizungumza baada washindi hao kula kiapo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa Mji, Majaliwa Said amewaasa viongozi hao kwenda kuwatumia wananchi ipasavyo bila kujali vyama vyao vya kisiasa.
Aidha, viongozi hao wapya wamepata semina maalumu iliyolenga kuelimisha kuhusu majukumu yao, ili kuwawezesha kutekeleza kazi zao kwa ufanisi na kuwa mfano bora katika utawala wa serikali za mitaa. Semina hiyo ilijumuisha masuala mbalimbali, ikiwemo sheria na taratibu za utawala, mikakati ya maendeleo, na njia bora za kushirikiana na jamii ili kufanikisha malengo ya maendeleo.