Pre GE2025 Dodoma: Yanayojiri Miaka 48 ya Maadhimisho ya Kuzaliwa kwa CCM

Pre GE2025 Dodoma: Yanayojiri Miaka 48 ya Maadhimisho ya Kuzaliwa kwa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Leo ndio ile siku ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM baada ya kuona matangazo mengi toka kwa chawa wa mama.

Watakuja na kubwa gani leo, wacha tuone.


Huyu hapa msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz akiwa anaingia kutumbuiza kwenye maadhimisho a miaka 48 ya CCM


Rais SamiaSuluhu Hassan alivyoingia na ulinzi mzito kshishiriki sherehe miaka 48 ya CCM, apigiwa shangwe


Rais Samia na Mwenyekiti wa CCM amesema pamoja na kuwa CCM kuwa Chama kikubwa na wanamatumaini makubwa katika Uchaguzi ujao ila hawapaswi kubweteka

"Ndugu zangu pamoja na hali hiyo ya kujiamini na kwamba CCM ndio Chama kikubwa na tuna matumaini makubwa kwenye uchaguzi ujao, tusibweteke. Tunatimiza miaka 48 katika mwaka wenye vuguvugu la uchaguzi mkuu nchi, kama nilivyosema katika mkutano mkuu uliopita hivi karibuni tusiruhusu kunyemelewa na kiburi cha kuwabeza wapinzani wetu lakini pia tusiingiwe na pepo la kuwaogopa"

"Kesho salama ya Chama chetu na Nchi yetu itahakikishwa kwa vijana wetu kujengewa uwezo ndani na nje ya nchi ili waweze kujipanga kitaasisi na waweze kupambana kwa hoja na yeyote mwenye hoja hasi kwetu, lazima umoja wa vijana wa CCM waendelee kuimarishwa kimkakati kwani hawa ni hazina ya chama, lazima wajengewe uwezo, wapikwe kiitikadi na katika mazingira ya dunia ya sasa, hawa wakikuwa ndio wanaoimarisha jumuia za UWT na Wazazi"

Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025

"Tuapoelekea katika uchaguzi mkuu, tutaendelea kujiimarisha zaidi ndani ya Chama, tumekiwezesha chama nyenzo muhimu za usafiri, tunataka kuona viongozi wa CCM wanawafikia Wananchi kuwasikiliza na kutatua changamoto zao, lakini katika hatua nyingine kichama tumejipanga na matumizi ya Tehama ili kukuza mawasiliano au kurahisisha mawasiliano, Chama sasa makao makuu wanaweza kuzungumza kwa kuonana, Katibu Mkuu anaweza kushiriki mkutano wa Kamati ya Siasa kwenye mkoa kwa kuonana"

"Nawahakikishia wanachama wa CCM na wananchi wote kuwa haki itatendeka katika kupata wagombea wa chama, tutawapa wananchi wepesi wa kuweka 'mafiga matatu"

Pia soma: Pre GE2025 - UWT: Tundu Lissu zungumza na Rais kwa staha, vinginevyo...
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-02-05 at 15.38.00_d3b39417.jpg
    WhatsApp Image 2025-02-05 at 15.38.00_d3b39417.jpg
    446.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-02-05 at 15.37.58_2ddc8bc0.jpg
    WhatsApp Image 2025-02-05 at 15.37.58_2ddc8bc0.jpg
    1 MB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-05 at 15.38.01_fc9db998.jpg
    WhatsApp Image 2025-02-05 at 15.38.01_fc9db998.jpg
    817.2 KB · Views: 4
Ila CCM wanatia huruma Sana kwanini wanatumia nguvu kubwa za kijinga?
 
Heri ya siku ya kuzaliwa UKOLONI/UBEBERU mweusi au ukoloni wa ndani. Tunapopongezana kwa kuzaliwa UKOLONI huu ni muhimu pia kutafakari ni kwa namna gani tunaweza kujinasua na ukoloni huu.
Tena afadhali ya Mkoloni, huyu ni katili kuliko kiama.
 
Katibu Mkuu wa CCM na Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wanachama, Wakereketwa na Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Kuzaliwa kwa CCM ; Jamhuri Dodoma.
 

Attachments

  • 20250205_150017.jpg
    20250205_150017.jpg
    68 KB · Views: 3
  • 20250205_150019.jpg
    20250205_150019.jpg
    64.1 KB · Views: 2
  • 20250205_150021.jpg
    20250205_150021.jpg
    70.8 KB · Views: 3
Back
Top Bottom