Dogo amegoma kwenda shule

stranger man

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
420
Reaction score
524
Wadau nina rafiki yangu hapa tunasota nae kitaa ye ana miaka 3 ana mdogo wake yupo form three mchepuo wa art leo amegoma kwenda shule amemwambia kuwa kama kaka yake amemaliza chuo kikuu akiwa anapata division one kuanzia form 4 mpaka six na chuo kafaulu vizuri.

Lakini ameishia kumuamsha dogo asubuhi kwenda shule akiwa hana kazi wakati yeye dogo akiwa huwezo wa kufaulu hana ameamua akache shule aanze kujiajili.
 
poa mwambie aendelee kukaa nyumbani asubiri kuolewa,shule haina dili kabisaa
 
Wasomi wenyewe washatosha tayari, hayo madegree ya arts/social sciences yana kazi gani tena kwenye soko la ajira?
 

Mwambie amwache aendelee tu kulala !

something blind bind in ur mind make it kind!!!
 
Sasa hivi mhitimu wa veta ana thamani kuliko mwenye degree
 
Mpeni ushauri ili aende shule;
Huyo kaka yake ipo siku atapata tu ajira.
 
Kwa upande wangu naona maamuzi ya huyo Dogo yapo sahihi kabisa,kwa sababu leo umuhimu wa elimu ni kuajiriwa tu, na toka udogoni unahusiwa kusoma kwa maana ndiyo njia pekee ya kupata maisha mazuri(wasio soma ndiyo wanastahili maisha mabaya) sasa anapokuja kuona mambo tofauti unategemea achukue uwamuzi gani, tena anajijua kabisa kuwa akili za darasani ni shida!!
 
Dogo amechukua maamuzi sahihi kabisa, bora aanze kujiajiri mapema.
 
At least amalize kidato cha nne then ajiajiri..
 
dogo kafikiria vizuri....ila atleast angemaliza form 4,later on mambo yakikaa vizuri akitaka kurudi shule...awe na pa kuanzia.
 
"huenda anajipanga kugombea ubunge mbeleni ambao hauhtaj kiwango chochote cha elimu as long as anajua kusoma na kuandika kiswahili na kiingilishi"
 

Kama dogo kagoma basi braza wake achukue madaftari ya dogo aende skul kwa dogo apige msuli.huyo dogo hana tatizo mbona hata bwakila yupo hivyo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…