.
Rapper mdogo kutoka A town Dogo Janja aliekua akisoma na kuishi Dar es salaam amerudishwa kwa wazazi wake Arusha jana kutokana na kufanya mambo mbalimbali ambayo uongozi wa Tiptop Connection haujapendezwa nayo.
Tip Top ambao walikua wanasimamia kazi za muziki za Janja wamempandisha basi na kumrudisha kwao jana baada ya kuona msanii huyo hazingatii shule kama inavyotakiwa, amekua mtoro wa mara kwa mara katika shule aliyokua akisoma ya Makongo na hasikii anaporekebishwa, hiyo ndio sababu kubwa ya kumrudisha ili kukwepa lawama za baadae ambazo zingetokana na Dogo Janja kutosimamiwa vizuri kwenye swala la Elimu kwa sababu Tiptop ndio waliokabidhiwa kumsimamia.
Stori kamili ya hii ishu utaipata baadae baada ya kuzungumza na Meneja wake ambae ni Madee.

Alichokiandika Dogo Janja kwenye Facebook jana.
thanks.....
Millard Ayo
Dogo Janja: Show ya
milioni, Madee alinipa laki
moja
Siku moja baada ya Dogo
Janja kudaiwa kufukuzwa
Tip Top Connection, ukweli
halisi kuhusiana na uamuzi
huo umewekwa wazi na
yeye mwenyewe.
Sababu zilizotajwa na Tip
Top Connection ni kwamba
Dogo Janja alilewa sifa na
kuwa mtoro shuleni.
Kwa mujibu wa interview
(ya pili kufanyiwa baada ya
kipindi cha Amplifaya cha
jana) tuliyofanya naye kwa
simu saa moja asubuhi leo
(June 14) akiwa stand
kurejea nyumbani, uonevu
na dhuluma ndivyo
vilivyomchosha kuishi Dar
es Salaam.
Anasema tangu aje Dar es
Salaam hajawahi
kusaidiwa chochote na
Madee zaidi ya mambo ya
muziki pekee huku kula,
malazi na ada ya shule
vikifanywa na rafiki yake
Madee aitwaye Abdallah
Doka ambaye (Dogo Janja)
alikuwa akiishi kwake.
Anasema kutokana na
ngoma zake kujipatia
umaarufu alikuwa akipata
show nyingi nchini na zote
alikuwa halipwi chini ya
milioni moja.
Kilichokuwa kinamsikitisha
anasema ni kulipwa hela
kidogo isiyozidi laki mbili
na hivyo kumfanya aishi
kwa tabu licha ya kuingiza
hela nyingi za show.
Nilikuwa navumilia tu bro
kwasababu kila
nilipolalamika kuhusu
mambo ya hela Madee
alikuwa mkali sana,
ameongea uchungu.
Dogo anasema ilikuwa
inafikia wakati akifanya
show za ukumbuni
hulipwa elfu hamsini au
chini ya hapo na wakati
mwingine alikuwa halipwi
kabisa.
Tamaa ilizidi kumwingia
Madee kiasi cha
kumnyanganya kadi yake
ya benki na kuanza
kuchukua hela bila kujua
password aliipata wapi.
Kuna wakati nilikuwa
nataka kumtumia mama
laki moja, Madee
akanikataza eti kwakuwa
watadhani nina hela sana,
anasema.
Mpaka tunaongea naye
asubuhi hii, anasema kadi
yake imebakiwa na shilingi
25,000 tu.
Ameendelea kudai kuwa
juzi Madee alimpigia simu
na kumwambia kuwa kaka
yake wa Kibaha ameandaa
show ya CCM na atamlipa
shilingi laki moja.
Hivi kweli bro mimi ni
mtu wa kufanya show ya
laki moja?. Hata hivyo
aliamua kukubali ili
kuepusha lawama.
Baada ya show kumalizika
anasema yeye na back up
artist wake walirudishwa
saa saba usiku wakati
asubuhi yake alitakiwa
kwenda shuleni kuchukua
namba ya mtihani na
kuandaa dawati la kukalia.
Dogo Janja anaeleza kuwa
inamuuma sana kwakuwa
muziki haujampa chochote
licha ya Madee ambaye
huwa hapati hata show
kumtumia kimaslahi na
hadi leo hii anamalizia
kujenga nyumba yake.
Ni kama vile Madee
alinipanda ili anivune.
Ameendelea kusema kuwa
hiyo juzi sasa hadi kufikia
Tip Top watangaze
kumfukuza alikuwa kwa
Tundaman akipiga story na
Madee akamuita kisha
kuanza kumpiga.
Alichukua simu yake
akaondoka nayo. Jamaa
alianza kujitumia meseji
kutoka kwenye simu
yangu kwenda kwake za
matusi ama kuwa nataka
kumroga. Jana
nimemuonesha Milard hizo
meseji na amesikitika
sana.
Anasema simu yake
alipewa jana.
Kitendo cha kumwambia
Madee kuwa amechoka na
anataka kurudi nyumbani
ndicho kimemfanya
amfanyie yote hayo hadi
kumwambia kuwa
watahakikisha
wanambania asifanye
vizuri tena kwenye muziki.
Pia amedai kuwa Madee
aliwapigia simu wazazi
wake ili wamkataze Dogo
Janja asifanye interview na
vyombo vya habari.
Wanajua nikiongea
wataabika sana. http://
leotainment.blogspot.com/2012/06/
dogo-janja-show-ya-
milioni-madee.html?m=1