Doing Business 2011 data for Tanzania, tumeanguka nafasi 3 tena!

Aibuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!. Kuna nchi ndogo nyingi zinafanya vizuri kasoro bongoland. Nchi nyingi za Afrika ya kati na kusini zinategemea bandari ya Dar pengine na Tanga lakini tunashindwa kujiinua jamani sisi ni washika mkia kila siku looh! Hii nchi ililogwa tangu ilipozaliwa duh
 
Mkuu Pakawa,

Ufisadi (Corruption) kwa mawazo yangu unachangia mambo mengi, mojawapo ni mambo kama haya. Tatizo wengi tafsiri ya ufisadi tunaichukulia vingine, lakini urasimu pia ni sehemu ya ufisadi tu, unafanyiwa urasimu wa kila namna ili utoe rushwa!

Masikini nchi yangu...
 
hii ni kweli kabisa maana nina watu wa karibu waliojaribu kuanzisha biashara! Kuna ukiritimba mwingi na milolongo kibao, hasa kwa wazawa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…