Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,086
- 2,823
Katika uzinduzi wa kiwanda cha Phillip-Morris, Morogoro, Rais wetu Dokta Magufuli, alirudia kuyakosoa mafuta ya kula yanayoletwa nchini kwamba hatujui kilichomo ndio maana tunapata ma kansa.
Lakini kwa miaka takriban 20-30 iliyopita hakuna kampuni inayoongoza duniani kwa kukosolewa, kushitakiwa na kulipishwa mabilioni ya dola kama Phillip-Morris kwa vile bidhaa yao inasababisha saratani.
Binafsi nakubaliana kabisa na vita dhidi ya imports zisizokuwa za lazima kama mafuta ya kula ambayo yanatufanya tusijenge viwanda vyetu.
Lakini ni kipi kinasababisha zaidi saratani, mafuta ya kula au sigara? Hatujui kwamba saratani ya koromeo na mapafu- saratani ya sigara- ndio inaongoza duniania kuua kuliko kansa zote?
Kwa Rais mwana-sayansi, mkemia bingwa, anaesema anawapenda sana watu wake, Phillip-Morris na wazungu wao wanatucheka sana kuona mtu huyo huyo anatusokomezea kooni li kiwanda la sigara!