Dokta Magufuli: Kipi kinaleta kansa, imports za mafuta ya kula au kiwanda cha sigara?

Tindikali

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2010
Posts
2,086
Reaction score
2,823


Katika uzinduzi wa kiwanda cha Phillip-Morris, Morogoro, Rais wetu Dokta Magufuli, alirudia kuyakosoa mafuta ya kula yanayoletwa nchini kwamba hatujui kilichomo ndio maana tunapata ma kansa.

Lakini kwa miaka takriban 20-30 iliyopita hakuna kampuni inayoongoza duniani kwa kukosolewa, kushitakiwa na kulipishwa mabilioni ya dola kama Phillip-Morris kwa vile bidhaa yao inasababisha saratani.

Binafsi nakubaliana kabisa na vita dhidi ya imports zisizokuwa za lazima kama mafuta ya kula ambayo yanatufanya tusijenge viwanda vyetu.

Lakini ni kipi kinasababisha zaidi saratani, mafuta ya kula au sigara? Hatujui kwamba saratani ya koromeo na mapafu- saratani ya sigara- ndio inaongoza duniania kuua kuliko kansa zote?

Kwa Rais mwana-sayansi, mkemia bingwa, anaesema anawapenda sana watu wake, Phillip-Morris na wazungu wao wanatucheka sana kuona mtu huyo huyo anatusokomezea kooni li kiwanda la sigara!

 

Dah watakuja vibwengo kuukosoa uzi wako
 
Elimu..., Elimu...., Elimu
Hii dhana kuna siku watu wataielewa tu.

mimi nadhani walikosea kuondoa mitihani ya Cambridge. Ilikuwa inafukanya unafikiri kabla ya kujibu swali, na ilijenga upeo wa raia.

Kingine, Mwalimu alikosea kufunga nchi, jinsi ilivyokuwa ni haiwezekani kupata passport bila idhini ya Mwalimu, na jinsi habari za nje zilivyokuwa marufuku nchini, ilikuwa ni kesi ya Usalama wa Taifa kukutwa na satellite dish, kwa mfano, japo yeye alikuwa nalo Msasani na Butiama.

Kwa hiyo waliua makusudi curiosity ya raia kujua nini kinaendelea duniani, ndio unakuta kampuni ya Phillip Morris hakuna mwanakijiji anaejua zahma lake la kusambaza kansa ulimwenguni, akiwemo Rais mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…