Dola ya Mrima(Kilwa) iliokuwa Taifa kuu Afrika Karne ya 10(1070 A.D)

Qwi Qwi Qwi...... yani jamaa kajifunga vibaya mnoo. Meli zimekua majabali na wasaliti wamekua vichuguu na bado wakapigwa!? Hii ni kudhalilisha Bara la Africa.
Yaani jamaa wamekua waongo waongo sana, halafu eti waafrika tunaonewa, mara tulikua na maendeleo ila hawataki kusema ukweli. Kwa simulizi hizo kama hiyo hapo unaona kabisa kuwa wenzao walikua more advanced kuliko wao. Jiulize hao wasaliti wali communicate kwa lugha ipi na hao wareni na kwa nia ipi wakati hata simu hazikuwepo? walijua wareno watarudi lini? Nani aliwaambia kuwa wapo njiani? Wamelalamika sana eti historia imefichwa, wanapewa nafasi ya kuifichua hiyo historia iliyofichwa wanaanza kutuletea 'Paukwa Pakawa'.
Ila kitendo cha waafrika na waarabu kushambuliwa, kupigwa na kushindwa vita dhidi ya miamba na vichuguu, hii ni kiboko.
 
Nafuatia kwa shauku maandishi yako ndugu. Unafanya vizuri sana. Lakini ili uwe credible na unachoandika kithaminiwe, itabidi ufanye bidii ya kusahihisha makosa mengi ya sarufi ya Kiswahili. Pia ufanye utafiti wa tarehe. Nitatoa mifano. Inaudhi na kwa kweli kupoteza ladha ya elimu unapokosea sana herufi za L na R na pia Z na DH.
Utajili (utajiri) mashaliki (mashariki)Sulutani (Sultani) Usambala (Usambara) habali (habari) Linajiimalisha (jiimarisha) Pia Kazaa (kadhaa) Andeni (Handeni) Na haya ni mistari michache ya juu tu!
Kuhusu tarehe unasema Dola ya Ottoman ilikuwa katika mwaka ya 680 AD. Ukweli ni kuwa mwaka huo ndiyo mwaka alipouawa Hussein bin Ali, mjukuu wa Mtume Mohammad SWA kule Karbala, Iraq. Mauaji yake yalileta tafaruku kubwa katika Dola la Kiislamu ambalo hadi wakati huo lilikuwa likiongozwa na koo mbili Bani Umayya huko Syria na Iraq, wakati Hijaz (Makka na Madina) ulikuwa ukoo wa Quraysh ukiwakilishwa na Hussein bin Ali. Dola ya Ottoman ilikuja nyuma sana na kwa kweli ilianza mwaka 1299 kwa huyo Osman mwenyewe kutwaa madaraka. Mwaka 1453 dola hiyo ilikamata Constantinople (Istanbul) yaliyokuwa makao makuu ya Kanisa la Mashariki (Eastern Orthodox), na wakahamishia makao makuu ya dola la Ottoman hapo.
 
Mimi mwaka 2014 nilitembelea cairo misri sekta ya Hiyo[emoji115][emoji115][emoji115] pekee inachangi 47% ya pato la taifa kalibu milioni 23$ kwa mwaka
Hivyo na sisi tuna haja ya kuwekeza kwenye hiyo sector ya urithi huu
 
Wanasiasa wanajua vizuri historia ya nchi yetu ilipo,ilipotoka na hata pengine inapoelekea..mimi nahisi wanaficha hiyo history ili tusisanuke ili waendelee kutupiga tu.
 
hata firauni alizidiwa? nasikia huko afrika magharibi kulikuwa na tawala tajiri ya dhahabu kuliko kokote duniani, hebu tueleze
AFRIKA ni bala ambalo kimsingi Lina historia yake. Tena yenye utajili na bakhishishi nyingi wrote wana tambua kuwa dola ya misiri ndio ilikuwa eneo la ustaalabu duniani. Pia kuna dola kama Songhai, Mali, na dola zingine nyingi ambazo zilikuwa na historia kuntu kabisa
 
UKITAKA KUJUA WATU WANAPUUZA MAMBO NENDA KILWA LEO HATA BILA TAKWIMU HUWENDA NI MIONGONI MWA WILAYA MASIKINI KABISA TANZANIA
 
KUNA UPOTOSHAJI MKUBWA WA HISTORIA JUU YA MILIKI YA KILWA HUSUSANI KUSHABIHISHA UARABU HIVYO WENGI KUKIMBILIA KUFUNZA KUWA NI DOLA YA KIARABU. HAYA YOTE MARA ZOTE YAMECHANGIWA NA DHANA ZINAZOLETWA IMA NA WAARABU(KWA MASLAHI YAO) AU WATU WASIOKUWA WAISLAMU KWA KUUVIKA UISLAMU UARABU. HAKUNA SHAKA KUWA UISLAMU ULIASISIWA KATIKA ARDHI YA WAARABU NA MTU AMBAYE NI MWARABU PASI SHAKA LAKINI WATU BAADAYE WATU WALIIONGOKEA DINI HIYO KWA SABABU TOFAUTI IKIWEPO UVAMIZI NA MAUAJI YA KIVITA(KASKAZINI YA AFRIKA KUTOKEA MISRI MPAKA MEGREB WALIKUTWA NA MBINU HIYO),BIASHARA IKIWEPO BIASHARA YA KAWAIDA NA BIASHARA YA UTUMWA FUATILIA NJIA WALIZOPITA WAARABU HATA HAPA TANZANIA URATHI WA UISLAMU UMESHAMIRI PIA USHAWISHI WA AINA NYINGINE. HIVYO KILA DOLA ILIYOKUWA YA WAISLAMU ILIKUWA NI YA WAARABU! MKUMBUKENI IBN BATUTA KISHA KASOMENI ACCOUNTS ZAKE ALIPOFIKA KILWA ALIANDIKA NINI(TUWE TUNAPEANA ASSIGNMENT ILI TUSILEMEZANE) LAKINI HATA LEO WAKAAZI WA KILWA KWA MAJORITY NI WAAFRIKA TENA TOFAUTI HATA NA BAGAMOYO ,PANGANI NA MIJI MINGI YA PWANI AMBAYO WAARABU WALIWEKEZA MAKAAZI YAO KIPINDI CHA MWISHO CHA BIASHARA YA UTUMWA HUSUSANI KUANZIA KARNE YA 16,17,18 na 19. KILWA ILIKUWEPO MAPEMA MNO KABLA LONDON HAIJAKUWA LONDON YA WAKATI WA MAPINDUZI YA VIWANDA KARNE YA 17 NA KILWA NI DOLA YA WATU WEUSI AMBAO HUENDA PASI SHAKA NDIO WAMWERA,WAMATUMBI,WANDENGEREKO HATA WANGINDO NA WENGINE WANOZUNGUKA MAENEO YALE TULICHOPOTEZA NI KUWA UKOLONI ULIFUNDISHA NA UKAELEWEKA WEMA KUWA MAMBO MAKUBWA YASINGEWEZA NA HAYAWEZI KUFANYA NA MTU MWEUSI HIVYO HATUNA UWEZO WA KUJIAMINI,PENYE ELEMENTI ZA UISLAMU TUTASEMA KILIKUWA CHA WAARABU, CHENYE ELEMENT ZA KIKRISTO TUTASEMA KILIKUWA CHA WAZUNGU. LAKINI HAKUNA ANAYEWEZA KUSEMA MACHANGO NA URATHI WA MAFANIKIO YA MWAFRIKO YANAYOHODHIWA NA YALIFANIKISHA KUWAA MWANGA WAZUNGU,WAARABU,WAAJEMI HATA WATU WA MASHARIKI YA MBALI KUAZNIA SHINARI(SUMERI),ASHURU(ASSYRIA),UAJEMI(PERSIA,),BABELI(BABYLON),UYUNANI(UGIRIKI),RUMI(UITALIANO),FONISIA(LEBANON) NA KOTE ULIMWENGUNI. kILWA NI DOLA YA WAAFRIKA. MIMI SI MUISLAMU,PIA SI MKRISTU MIMI NI MUAFRIKA KILICHOFANYWA NA WAAFRIKA SIJALI DINI YAO KUWA NDIO MSINGI WA UWEZO WAO BALI NI KIPAWA CHA MUNGU WETU AMBAYE NI MKUBWA KULIKO DHANA ZOTE ZA IMANI
 
 
kuhusu cita vya Umuhayya umekosea na kupotosa pia,hakikuwa kipindi cha Ottoman Empire iliyoanzishwa na Uthman wa uturuki kwa kuwa ndie muasisi wa Ottoman empire na si Khalifa Uthman khalifa wa 3 wa uislamu baada ya Abubakr, na Umar .lakini Ottoman Empire ilianza Uturuki(Eneo lililokuwa likiitwa Anatolia) karne ya 14 na mwasisi wake ni Osman I au Othman ambaye jina lake ndio ilipewa dola aliyoiasisi kuanzia karne ya 14 nad ndio dola kubwa ya mwisho ya kiislamu iliyokufa 1921 na kuanzishwa taifa la Uturuki ya leo. hoja hii imeleta mkanganyiko mkubwa sana hususani kwa wanahistoria uchwara ambao hudhani ukijua uislamu basi umeijua na historia ya uislamu hsusani kusambaa kwake. Hivyo dola la Ottomani halikuanza karne ya 7 wala halikuanzishwa na Khalifa uthman bali. lilianza karne ya 14 na liliasisiwa na osman i muumini wa madhehebu ya Kisufiani kipindi ambacho wamongoli walipiga miji mingi ya kiislamu ikiwepo basra iraq katika kujitanua kwao .Tuwe makini
 
Inaonekana tumetawaliwa kwa zaidi ya milenia. Kupata ukweli kabla ya waarabu na wazungu itakuwa kazi sana.
 
Heshima kwako mkuu, hivi vitu adimu kabisa.
 

Watasema uchochezi huo wanafunzi wa Sheikh Mohamed Said wanashindwa kutetea hoja zao dhaifu.Ikiwa duwaa ilikuwa na nguvu kiasi cha kuzigeuza merikebu za wareno kuwa miamba ni kwanini Wareno waliwatawala ??????.Hizo ni hadith za kuchangamsha barza baada ya kunywa gahawa na visheti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…