Dola ya wachaga kabla ya uhuru

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
240
Reaction score
767
DOLA YA WACHAGGA MIAKA MICHACHE KABLA YA UHURU.

By Malisa GJ,

Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfumo rasmi wa uongozi. Wao waliziita tawala za jadi (Chiefdoms).

Moja ya tawala iliyokua na nguvu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ni dola ya wachagga (Chagga state). Zilikuwepo nyingine zenye nguvu kama Himaya ya Sultani wa Zanzibar, Dola ya Buganda, Nyamwezi, Ngoni, Haya, Hutu, Tutsi, Hehe, etc.

Dola ya wachagga imetamalaki eneo la pembezoni mwa mlima Kilimanjaro kuanzia maeneo ya Rongai hadi Siha.

Eneo hili lilikua na mtawala mkuu mmoja (aliyeitwa Mangi Mkuu). Huyu alikua kama Rais ama Mfalme wa jamii hiyo. Chini yake walikuwepo watawala wakuu wawakilishi wa majimbo. Hawa waliitwa 'Mangi Waitori'. Chini yao walikuwepo watawala wa wa maeneo madogo, hawa waliitwa Mangi kama vile Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri etc.

Kwa mfano eneo kama Rombo lilikuwa na Mangi wengi. Alikuwepo Mangi wa Keni, Mangi wa Mashati, Mangi wa Mengwe etc. Lakini wote waliunganishwa na Mangi Mwitori wa Rombo. Vivyo hivyo katika maeneo ya Kibosho, Machame, Siha, Old Moshi, Marangu etc.

Mangi mdogo aliripoti kwa Mangi Mwitori. Mangi Mwitori naye aliripoti kwa Mangi Mkuu aliyeunganisha wachagga wote.

Kwa mfano kufikia mwaka 1953 Mangi Mwitori wa Vunjo alikua Petro Itosi Marealle, Mangi Mwitori wa Hai alikua Abdiel Shangali, Mangi Mwitori wa Rombo alikua James Selengia Kinabo kabla ya kustaafu mwaka 1952 na John Maruma kuchukua nafasi yake.

Mangi Mwitori alichaguliwa na wamangi wadogo. Kisha wamangi wadogo na wamangi waitori waliunda baraza kuu la uongozi (Supreme council) ambalo lilimchagua Mangi Mkuu.

January 1952 kulifanyika uchaguzi wa kumchagua Mangi Mkuu wa Wachagga. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu (Old Moshi), Petro Marealle wa Vunjo, John Maruma wa Rombo, na Thomas Marealle wa Marangu.

Baada ya kila mgombea kunadi sera zake, hatimaye kura zilipigwa na Mangi Thomas Marealle kutangazwa mshindi, akifuatiwa kwa mbali na ndugu yake Mangi Petro Itosi Marealle, aliyekuwa Mangi Mwitori wa Vunjo.

Mangi Mkuu ndiye aliyekuwa Kiongozi mkuu wa dola ya wachagga. Baraza la uongozi (Supreme council) ndicho kilikua chombo cha juu kinachosimamia utendaji wa serikali.

Kwahiyo Mangi mkuu alijitahidi sana kushirikiana mangi waitori na mangi wadogo kuhakikisha jamii nzima ya wachagga inajiletea maendeleo.

Kila Mangi alikua na baraza lake la ushauri lililojulikana kama 'baraza la wachili', ambalo lilifanya kazi kama baraza la mawaziri kwa sasa.

Ushirikiano huu ulifanya dola ya Wachagga kupiga hatua kubwa kimaendeleo kuliko jamii nyingi za wakati huo.

Kwa mfano kufikia mwaka 1920 dola ya wachagga ilikua ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kuanzisha na kumiliki gazeti lake (Komkya). Miaka 10 baadae dola ya Buganda (Buganda Kingdom) nayo ilianzisha gazeti lake (Buruuli) na mwaka 1940 Himaya ya Sultani wa Zanzibar (Zanzibar Sultanate) nayo ikaanzisha jarida lake (Imperial).

Si hivyo tu, huduma za maji, umeme, miundombinu ya barabara, hospitali na shule vilifika mapema kulinganisha na maeneo mengine ya nchi. Ikulu ya kisasa ya Mangi Mkuu wa wachagga, iliyojengwa karibu miaka 100 iliyopita ndiyo inayotumika hadi sasa kama Ikulu ndogo ya Rais kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Zilizokuwa ofisi za watendaji wa serikali ya Mangi mkuu (eneo la KDC Moshi) ndio ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Moshi kwa sasa.

Maendeleo haya na mengine mengi, wachagga waliamini yalitokana na elimu. Kwahiyo mwamko wa elimu ulikua mkubwa hasa baada ya wamisionari kujenga shule na huduma za afya kila walipojenga kanisa. Vitu hivi vitatu viliambatana. Kanisa, Shule, na Kituo cha afya.

Kwahiyo hata kwenye kuchagua viongozi, yule aliyekuwa na elimu nzuri ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda ikiaminika kwamba elimu yake itachochea kasi ya maendeleo. Na hii ni moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha umangi mkuu mwaka 1952, kwani kati ya wagombea wote yeye ndiye aliyekua na shahada ya uzamili (masters degree) kwa wakati huo.

Kabla ya uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na mzee Fredrick Mchauru ambaye walisoma pamoja London School of Economics, kabla ya Marealle kupata ufadhili Cambridge University (Trinity College).

Iliaminika pia kwamba Uingereza ilitaka dola ya wachagga ijitenge kutoka Tanganyika na itafute uhuru wake yenyewe, kama Rwanda na Burundi zilivyojitenga kutoka Tanganyika baada ya vita vya kwanza vya dunia, wakati huo zikiitwa Ruanda-Urundi.

Hata hivyo mpango huo ulishindikana kwa kuwa Tanganyika ilikua 'Trusteeship colony' ya Umoja wa mataifa, na Uingereza alikabidhiwa tu aisimamie hadi iweze kujitawala. Kwahiyo hoja ya Muingereza ilitupwa kwa maelezo kwamba wakati wa kugawanya bara la Afrika pale Berlin mwaka 1984/85 hakuna nchi inayoitwa 'Chagga state' iliyogawanywa. Hivyo uhuru unaopaswa kuwa wa Tanganyika kwa ujumla na sio wa jamii moja moja.

Baada ya jaribio hilo kushindwa, inadaiwa shirika la ujasusi la Uingereza (M16) lilimpendekeza Mangi Thomas Mareale kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya uhuru.

Katika moja ya barua za Richard Turnbull (Gavana wa mwisho wa Uingereza) kwenda kwa shirika la ujasusi la nchi hiyo (M16) ilieleza mapendekezo hayo kwa Thomas Mareale.

Sehemu ya nyaraka hiyo iliyoandikwa mwaka 1958 ilisema 'I consider Thomas Marreale an outstanding Chagga leader. I dont know him personally but he would be the leader of Tanganyika if British had to leave. However he lack support from other tribes'

Turnbull alikua akiwaelezea M16 kuhusu Mangi Thomas Marealle na umahiri wake katika uongozi. Hata hivyo alionesha hofu kuwa Marealle hakuwa na ushawishi mkubwa kwa makabila mengine nje ya wachagga.

Na hii ni moja ya hofu kubwa aliyokua nayo Mwalimu Nyerere wakati wa kudai uhuru. Alipofika uchaggani alikuta dola ya wachagga ina mamlaka kamili. Ilikua na 'well defined leadership structure', bendera yake, wimbo wake, na askari wake.

Nyerere alisema ili Tanganyika iwe uhuru lazima dola ya wachagga ife kwanza, kwa sababu hatuwezi kuwa na taifa moja ndani ya taifa jingine. Mwaka 1961 Nyerere aliagiza bendera ya Tanganyika isipandishwe kabla bendera ya wachagga haijashushwa kwanza. Tarehe 8 December 1961 saa 5 usiku bendera ya wachagga ilishushwa katika Ikulu ndogo ya Moshi, na muda mfupi baadae (saa 6 usiku, December 9) bendera ya Tanganyika ikapandishwa.

Hata hivyo hofu ya Nyerere haikua na mashiko kwa sababu Mareale mwenyewe alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa kudai Uhuru. Na ili kuonesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumhujumu, aliamua kujiuzulu nafasi yake ya umangi mkuu mwaka 1960, na kuruhusu askari wake kujiunga na jeshi la Tanganyika.

Pichani ni wagombea watatu kati ya watano walioshiriki uchaguzi wa Mangi Mkuu mwaka 1952. Kutoka kushoto ni Mangi Thomas Mareale aliyeshinda uchaguzi huo), Mangi John Maruma (Mangi Mwitori wa Rombo), na Abdieli Shangali (Mangi Mwitori wa Machame).

Malisa GJ
01/01/2019
Moshi.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie huyo mwandishi akajifunze vizuri.
1. Shirika la Ujasusi la Uingereza haliitwi M16 bali ni MI6. Nilidhani ni suala la typo tu lakini kinyume chake naona amerudia makosa yake tena na tena na kuleta maana kuwa kumbe si makosa bali ndiyo uelewa wake.
2. Wachaga si kabila pekee ambalo lilikua limeji establish kwa maana inayosimuliwa, kinachoonekana hapa ni wachaga kuomboleza na kuikumbuka historia ya hali ilivyokuwa miaka ile. Kuna sababu ya kilio chao cha hivi sasa wanapokazana kusimulia historia yao lakini miaka mingine iliyopita hakukuwa na kelele za wachaga kukazana kuandika kama sasa.

3. Kuna story nyingi za kuunga unga ili kuonekana wachaga walikua wanabembelezwa hado kushusha bendera yao ili ya Tanganyika ipande kitu ambacho si kweli.
4. Chief Doms ziliuawa.na hili ni kwa nchi nzima wala hakuna swala la Mangi Mkuu kijiuzuru ili kumpisha Nyerere aongoze. Alijiuzuru sababu hizo Chief Doms ziliachwa bila ya power yoyote ile kimaamuzi. Ndipo wakaleta janja nyingine za kuibukia kwenye vyama vya ushirika navyo wakatumwa watu wa system kwenda kuviua.

Msitake kupotosha watu kwa mambo ambayo hayakuwahi kuwepo.
 
Mkuu, nadhani magazeti yalikuwa mawiliyaani Komkya na Kusare??? Masalia yake yapo na hata jf ukisearch utayapata
Hata hivyo siopendaji historia kusoma historia km hizi kwani waandishi wake huandika yanayowapendeza wao. Mfano John Okello hatumsikii sana
 
Sehemu nyingi za Afrika zilikuwa na makabila yenye utawala mahsusi. Kwa mfano utawala uliokuwepo kabla ya wazungu ukanda ambao sasa ni Rwanda, Burundi na mkoa wa Kigoma ulikuwa na system mahili. Mkanganyiko uliojitokeza kati ya Watutsi na Wahutu huko Rwanda na Burundi ulileta mvurugano mbaya. Kwa upande wa mkoa wa Kigoma hali ya Burundi na Rwanda haikujitokeza kwa vile uamuzi wa serikali ya Nyerere kuondoa chiefdoms ndio sababu mojawapo kuu ya kuepusha tribal conflicts. Mimi naona hata hivyo inabidi historia kama hizi zifanyiwe utafiti na kufundishwa mashuleni na vyuoni.
Asante sana ndugu kwa kutuletea historia hii ya Wachaga.
 
Wanzungu ndo waliamua tuwe watanganyika na sisi tukawa.Wasingeamua tungekuwa nani? Sisi nje ya maamuzi ya wakoloni ni nani?
 
CDM kinachowaponza ni kuwa na watu wenye kuendekeza ukanda na historia za ajabu ajabu za kuunga unga zisizo na marejeo/reference kwa lengo la kufurahisha akili zao dhahania na hisia za kuonewa
 
Kipengele kinachonichekesha ni kwamba Alimpa ushirikiano nyerere kwenye harakati za kudai uhuru. Hilo sio kweli hata kidogo hawa wajamaa ni wabinafsi toka zama. Shukrani kwa Nyerere kwa kuondoa matabaka hawa jamaa wangekabidhiwa nchi tungeona maajabu i swear

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malisa hivi unajua wanaostahili kuitwa kabila la wachagga mkoani kilimanjaro ni wananchi wa eneo gani?
 
at least ume admit ukweli ambao hausemwi Sana kuwa Nyerere aliua cooperative societies n labour union maliciously
 
Kama leo kungekuwa na hiyo dola basi ingekuwa ni moja ya nchi maskini sana Duniani..
Ni landlocked, Ingekuwa ni nchi ya watu wajinga kuliko wotw, ingekuwa imejaa vita na vurugu za wenyewe wenyewe
 
Kama leo kungekuwa na hiyo dola basi ingekuwa ni moja ya nchi maskini sana Duniani..
Ni landlocked, Ingekuwa ni nchi ya watu wajinga kuliko wotw, ingekuwa imejaa vita na vurugu za wenyewe wenyewe
foolish comment
1. chaga state imepakana na Kenya, hence sio landlocked (nchi kuwa landlocked sio kigezo Cha kupima uchumi wa nchi)
2.before n after Uhuru himaya ya wachaga inaongoza kwa shule Bora na watu waliolimika
3.vurugu how n why
 
Hawapendi kuwa Watanzania. Wanatanani tena wawe na Mangi wao. Na hilo siyo kosa hata Wascot hawataki kuwa waEngland. Na wana masimulizi mazuri ya utawala wao ulivyokuwa bora kuliko huo walionao sasa kama wanavyofanya Wachaga. Sioni ajabu hawa Watu wa Kaskazini kukumbukia historia yao na kutamani kurudia tawala zao za zamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…