Dollar inaanza kupanda thamani dhidi ya Shilingi

Dollar inaanza kupanda thamani dhidi ya Shilingi

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Hapa katikati kumekua na mtiririko mkubwa na wa kushangaza wa kushuka kwa kiwango cha kubadilishia fedha hasa Dollar ya kimarekani dhidi ya Shilingi ya Tanzania.

Hali hiyo ilipelekea watu wengi kujiuliza maswali mengi na kukosa majibu. Wengi walifikiri labda ni matokeo ya uchaguzi wa Marekani yameathiri thamani ya dola, wengine wakafikiri ni benki kuu ya Marekani (Federal Reserve) kupunguza riba na wengine wakafikiri ni kuimarika kwa uchumi wa Tanzania na wengine wakafikiri ni kampeni ya de-dollarization ya BRICS nk.

Lakini ukweli ni kwamba kuanzia mwenzi October hadi December hua kunakua na kushuka kwa viwango vya kubadilishia fedha Tanzania kwa sababu kuu 2, sabau ya kwanza hua ni mauzo ya korosho nje ya nchi ambayo huingiza kiasi cha dollar milioni 200 nchini, hivyo kuongeza upatikanaji wa dollar kwenye soko la ndani na kupunguza viwango vya kubadilishia fedha.

Sababu nyingine ya pili hua ni mauzo ya dollar kwa kampuni za ndani zenye mapato ya dollar hasa kampuni za madini ili kuweza kulipa kodi na malipo mengine ya lazima nchini.

Kwa mtazamo huo, mwezi wa 11 mauzo ya korosho yaliingiza dollar kati ya 150m hadi 250m ana pia makampuni ya madini kama Geita na mwngine yameingiza sokoni kiasi cha dollar 130+m sokoni, hivyo kuongeza upatikanaji wa dollar nchini kwa karibu dollar milioni 400 (karibu TZS Trilioni 1) ndani ya kipindi cha miezi 2. Kumbuka soko letu la ndani halina uwezo wa kufyonza(absorb) kiwango kikubwa kama hicho cha fedha za kigeni kwa muda mfupi hivyo kwa wakati mmoja ukizingatia pia kwamba kipindi hicho watumiaji wakubwa wa dollar nchini hutakiwa kulipa kodi (hivyo hutunza shilingi ili kwanza walipe kodi). Hivyo kunakua na supply kubwa ya dollar halafu demand ya dollar hakuna.
FB_IMG_1734422517325.jpg
FB_IMG_1734422508650.jpg

Ukiangalia hizo picha 2 hapo juu ya tarehe 16 na leo utaona kiwango kikianza kupanda. Kwa sasa benki kuu inaauza dollar kwa 2,334 huku benki za biashara kiwango kikiwa ni 2,400. Hii ni trend ya kupanda ndio imeanza, trend hiyo itakuja kushuka tena kipindi kama hiki 2025.

Hivyo, kama una shilingi sasa ndio wakati mzuri wa kununua dollar kwa sababu soon kuanzia Januari kutakua na mahitaji makubwa sana ya Dollar kwa ajili ya kuagiza bidhaa nje ya nchi. Hii biashara ya kununua Dollar kipindi hiki halafu kuja kuuza kwa bei ghali ndio biashara inafanywa na wachina hapa nchini na wanapiga faida ya kufa mtu.

This is for your information and action. Asante
 
Back
Top Bottom