Mwanzoni watu wakiweka bei za bidhaa na services katika US Dollar kwa sababu ya kutokuwa na imani katika umadhubuti wa shilingi, hasa katika viwango vya kubadilisha fedha ukilinganisha na fedha za kigeni kama dola za Kimarekani.
Siku hizi ambapo dola inashuka, hii imekuwa siyo swala kubwa sana, imebaki kwa maoni yangu kwa sababu katika mipango ya muda mrefu, bado dola ya kimarekani inaonekana kuwa madhubuti zaidi ya shilingi, lakini vitu vingine vinavyopangiwa dola haviko katika mahesabu ya muda mrefu, na kwa kweli katika wakati huu ambao dola ya kimarekani inaweza kuwa inashuka thamani kwa kasi na kusababisha uwiano wake na Shilingi kuipa shilingi nguvu zaidi, mtu anayelipwa kwa shilingi kwa kufuata thamani ya dola anaweza kupunjwa.