Dome Okochi Budohi "Mau Mau" ndani ya TANU?

Dome Okochi Budohi "Mau Mau" ndani ya TANU?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
DOME OKOCHI BUDOHI "MAU MAU" NDANI YA TANU?

Kadi ya TANU ya Dome Budohi ni no. 6.

Dome Budohi alikuwa Mluya kutoka Kenya lakini alikuwa mwanachama na kiongozi wa TAA na hivi ndivyo alivyoweza kupata kadi hiyo no. 6.

Mimi nikimfahamu katika utoto wangu kwa jina la Dickson alipokuwa akija kwetu na kuingiliana sana na wazee wangu.

Pamoja na yeye walikuwa Wakenya wawili ambao wote niliwafahamu kwa majina yao ya kwanza tu, Maxwell na Martin.

Haukupita muda mrefu toka TANU iundwe Dome Budohi alikamatwa pamoja na Wakikuyu wengi waliokuwa Tanganyika kwa tuhuma za kuhusishwa na Mau Mau.

Wengi wa hawa Wakikuyu waliotiwa mbaroni walikuwa wafanya biashara Mwanza na sehemu nyingine ya Kanda ya Ziwa.

Martin alirudi Kenya lakini Maxwell alibaki Tanzania na mimi nilikuwa nikikutananae hadi katika miaka ya 1980.

Mara ya mwisho tulionana Mtaa wa Mafia na tulipiga picha pamoja.

Picha yangu na Mzee Maxwell hiyo hapo chini.

Ilikuwa Maxwell ndiye aliyefanya juhudi ya kunikutanisha na Dome Budohi Nairobi mwaka wa 1972 alipoona nataka sana kujua yale yaliyokuwapo Mtaa wa Kipata katika miaka ile ya kupigania uhuru.

Maxwell akiniambia kuwa Dome Budohi alikuwa mstari wa mbele katika TANU hadi mwaka wa 1955 aliposalitiwa na Martin kupitia barua iliyotoka Kenya kuja kwa Budohi barua ambayo ilimuhusisha na Mau Mau.

Budohi alikuwa akifanya kazi katika duka la muziki la Assanand lililokuwa Ring Street (sasa Mtaa wa Jamhuri) na alikuwa mmoja wa vijana wanamuziki akipiga drums katika Skylarks Band iliyokuwa ikiongozwa na Ally Sykes.

Martin alikuwa akipiga trumpet katika bendi hiyo iliyokuwa maarufu kwa vijana katika miaka ile ya 1950.

Budohi pia alikuwa muigizaji wa senema na aliigiza senema moja, "Mgeni Mwema," pamoja na Rashid Mfaume Kawawa.

Juu ya haya yote hawa vijana pamoja ya kuwa walikuwa hawapunguki katika kumbi mbili maarufu za Dar es Salaam ya wakati ule, Alexander na Arnautoglo walikuwa wapigania uhuru.

Nakumbuka kama.jana vile mazungumzo yangu na Dome Budohi nyumbani kwake Ruiru na kisha Ngei Estate alipohamia baadae.

Aliniambia kuwa alikitahidi sana kutafuta kuonana na Julius Nyerere wakumbushane enzi zao kila alipokuwa akienda Nairobi lakini hakufanikiwa.

Dome Budohi hakurudi tena Dar es Salaam hadi alipofariki.

Nimeshindwa kabisa kujua kwa uhakika kama Martin alikuwa kachero katika Special Branch au vipi.

Lakini itoshe tu kuwa katika kipindi hiki tunachokizungumza ilikuja kunidhihirikia baadae sana baada ya uhuru kuwa Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na mtu karibu sana na Abdul Sykes Secretary wa TAA alikuwa kachero wa Special Branch pamoja na Alexander Tobias.

Alexander Tobias alikuwa ameajiriwa na TAA mwaka wa 1950 kama Executive Secretary.

Picha: Kambi ya Mau Mau Kenya.

Screenshot_20210907-043436_WhatsApp.jpg


Screenshot_20210907-043414_WhatsApp.jpg


Screenshot_20210907-043412_WhatsApp.jpg


Screenshot_20210907-101203_WhatsApp.jpg
 
"Lakini itoshe tu kuwa katika kipindi hiki tunachokizungumza ilikuja kunidhihirikia baadae sana baada ya uhuru kuwa Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na mtu karibu sana na Abdul Sykes Secretary wa TAA alikuwa kachero wa Special Branch pamoja na Alexander Tobias"


Mzee Mohamed

Nimesoma ulichoandika hapo juu sioni kama kina uhusiano wowote na mada kuu ambayo imekusudiwa

Lakini nafahamu wazi kuwa huwezi andika chochote bila kuhusisha udini, na hi ndiyo rangi yako halisi

The inclusion of Ally Tambwe in the story as being undercover agent is not only ridiculously but also absurd
 
Mkuu

Naona umejaribu kua mganga kwa kujifanya kutaka kujua "intentions" za mwandishi

Huwezi kujua "intentions"za mwanadamu mwingine kwenye ubongo wake kama yeye hajasema kwa kinywa chake intentions zake.

Wewe umeamua kujipa cheo cha uaguzi kujaribu kuagua intentions zake wakati hajasema

Kwani kwenye story yake mbona kataja na majina ya wakristo?Au umeona ya Kiislamu tu?

Acheni sensitivity za kitoto hizi,ongelea real problems na sio hizi prejudices zenu kutokana na imani zenu mlizonazo kwenye bongo zenu.

Sisi wengine tusio na dini hatuoni huo upumbavu,tunaona majina mbalimbali ya wanadamu mbalimbali waliofanya mambo mbalimbali aliyoelezea muhusika

Ni Jambo la kawaida kwa binadamu kuwa na upeo tofauti wa kutambua masuala mbalimbali yaliyoandikwa ama kuwasilisha

Uchambuzi wako kwa yale uliyoyasoma ndiyo upeo wako.ulipogota
 
"Lakini itoshe tu kuwa katika kipindi hiki tunachokizungumza ilikuja kunidhihirikia baadae sana baada ya uhuru kuwa Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na mtu karibu sana na Abdul Sykes Secretary wa TAA alikuwa kachero wa Special Branch pamoja na Alexander Tobias"


Mzee Mohamed

Nimesoma ulichoandika hapo juu sioni kama kina uhusiano wowote na mada kuu ambayo imekusudiwa

Lakini nafahamu wazi kuwa huwezi andika chochote bila kuhusisha udini, na hi ndiyo rangi yako halisi

The inclusion of Ally Tambwe in the story is not only ridiculously but also absurd
Uzalendo...
Ikiwa umeona ikhtilafu hili ni jambo la kawaida baina ya watu.

Ama kuhusu Uislam hakika umesema kweli.

Lakini hiyo ndiyo historia ya TANU ambayo naamini hukupata kuisikia popote ila labda kama umesoma kitabu cha Abdul Sykes.
 
Back
Top Bottom