Du! Ndugu yangu utadhani ulikuwa kwenye mawazo yangu. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi jinsi watu wengi wasivyotumia akili zao kufikiri wale nini. Wengi wetu kinachotusukuma tule nini ni kile macho yanachokipenda, au kina test nzuri au kuiga jamii ya mastaa fulani wanakula nini, au kuangalia watu waliofanikiwa kiuchumi wanakula nini.
Sembe ni kati ya matokeo ya mfumo huu mbovu, watu wanalipa gharama kubwa kutokana na kutofikiria wanakula nini. Baada ya kuamia mjini nimejaribu kufanya uchunguzi wa maisha ya watu katika kula na nimegundua uzembe mkubwa wa nini tunachokula. Nimeogapa sana kula hotelini, kwa mama ntilie kununua vyakula vya supermarket n.k. Inaonekana ni namna fulani hivi ya ushamba au ulimbukeni lakini ni tahadhari tu. Nimejiandaa sasa hivi kula matunda kwa wingi, na raw foods kwa ujumla (nakwepa sana vyakula vya kupika)
Ukiangalia jinsi watu wanavyobugia mafuta, utashangaa sana, mtu anaamka asubuhi anakunywa chai ya maziwa kwa maandazi, saana nne kwa mayai ya kukaanga, mchana anakula chipsi mayai, jiuni anakula ndizi nyama rosti Mafuta ni lukuki hapo.
Badala yake angekula nyakumla mchemsho na matunda kama parachichi hivi, na karanga kidogo angekuwa amepata mafuta fresh ndani ya mwili wake. Mafuta mengi tunayotumia yametengenezwa kisanii mno.
Kuna mambo mengi sana ya kuangalia katika milo yetu. Leo hii unaweza kukutana na mtoto wa miaka kumi lakini kwenye kiti cha watu wawili kwenye daladala anakaa mwenyewe na kuoccupy nafasi yote kwa sababu ya unene, balaa kabisa.
NAKUUNGA MKONO MAN KUANZA KULIFANYIA KAZI ILI KUTENGENEZA PESA.