Donald Dombo Ngoma amesaini mkataba mpya wa miaka miwili Yanga SC

Donald Dombo Ngoma amesaini mkataba mpya wa miaka miwili Yanga SC

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
View attachment 531882
Kuna tetesi kwamba Donald Ngoma atania saini kwenye form za usajiri za Yanga mchana huu ili kuendelea kuitumikia Yanga,pia taarifa zinaendelea kusema kwamba,kiungo wa kati wa Yanga aliyevumishiwa kusaini Simba Haruna Niyonzima nayeye pia kaamua kujirudisha Yanga ili wakae mezani upya na kama watashindwana basi haoni sababu ya kuichezea timu nyingine ya Tanzania,na badala yake atafungasha virago vyake na kurejea kwao.
Taarifa zaidi zitafuatia.

======

UPDATES:

======

ATTACH=full]532001[/ATTACH]
IMG-20170628-WA0001.jpg
View attachment 531882 View attachment 531878
C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_ngoma3.jpg


Na Mahmiud Zubeiry, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC.
Ngoma aliwasili jana usiku Dar es Salaam baada ya taarifa kwamba amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Polokwane City ya Afrika Kusini.

Lakini tangu jana mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga kabla ya leo mchana kusaini, hivyo pia kuzima tetesi za kwamba anataka kujiunga na mahasimu, Simba.

Katika miaka yake miwili ya kwanza, Ngoma alikuwa ana msimu wa kwanza mzuri Yanga SC, akiiongoza kutwaa mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kuiwezesha pia kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ua kutolewa 16 Bora Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, msimu wake wa pili Ngoma hakuwa mzuri Yanga kutokana na kusakamwa na maumivu ya goti, huku timu yake ikiweza tu kutetea taji Ligi Kuu na kuvuliwa mengine ya Ngao ya Jamii iliyochukuliwa na Azam na ASFC lililobebwa na Simba.
Na hata katika michuano ya Afrika, Yanga haikuweza kurudia mafanikio yake ya msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi.
Ngoma aliyezaliwa Kwekwe, Zimbabwe alijiunga na Yanga SC mwaka 2015 akitokea FC Platinum ya kwao, aliyoanza kuichezea mwaka 2012 akitokea Monomotapa United iliyomuibua mwaka 2011.

Amewahi kuitwa timu ya taifa ya Zimbabwe mara kadhaa tangu mwaka 2011na hadi sasa amecheza mechi nane na kufunga mabao matatu. Na kwa kusaini Yanga, maana yake ataendelea kufanya kazi na rafiki zake, kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko na mshambuliaji Mzambia, Thabani Kamusoko
 
Mmmhh,, na zile taarifa za Ngoma kusaini miaka mitatu Polokwane fc ya south vipi??
 
baada ya kuhusishwa kujiunga na polokwane ya south africa, huku simba nao wakimvizia
hatimae donald ngoma aliingia jana usiku Tanzania na leo mchana amesaini mkataba wa miaka 2 wa kuendelea kuitumikia yanga
19554281_1451746991513362_2255551501798678627_n.jpeg
19437743_1451746921513369_7504989322394082045_n.jpeg

Ngoma alikuwa akisakwa na Simba kwa nguvu zote
 
Am
View attachment 531882
Kuna tetesi kwamba Donald Ngoma atania saini kwenye form za usajiri za Yanga mchana huu ili kuendelea kuitumikia Yanga,pia taarifa zinaendelea kusema kwamba,kiungo wa kati wa Yanga aliyevumishiwa kusaini Simba Haruna Niyonzima nayeye pia kaamua kujirudisha Yanga ili wakae mezani upya na kama watashindwana basi haoni sababu ya kuichezea timu nyingine ya Tanzania,na badala yake atafungasha virago vyake na kurejea kwao.
Taarifa zaidi zitafuatia.........
amwage tuu maana kipaji ni chake na atatumia atakavyo. Cha muhimu pesa
 
Back
Top Bottom