Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu watanzania,
Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa Donald Trump amemteua mgombea Mwenza wake Mwenye Umri wa Miaka 39 anayefahamika kama J.D Vance ambaye amewahi kutoa maneno makali sana kumtupia Trump mwaka 2016 wakati wa kinyang'anyiro cha Urais japo alikuja akajutia maneno yake miaka michache baadaye.
Mgombea Mwenza huyo kijana unaweza kusema ni kama mtoto wake Trump wa kumzaa. Maana kwa sasa Trump ana umri wa miaka 78 huku mpinzani wake Joe Biden ana umri wa miaka 81. Hapo ndio mtajua kuwa za kuambiwa changanya na za kwako maana angekuwa ni Muafrika ndio anagombea kwa umri huo ungesikia maneno ya kejeli kutoka kwa hawa mabeberu.
Jiulize je Marekani hakuna vijana wa kuongoza? Hakuna wasomi? Hakuna vijana wanaoaminika? Sasa huko vyuo vikuu wanakwenda kusomea nini? Kwanini vijana wa kimarekani hawaaminiki katika nafasi ya Urais?
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Kama kizungu kinapanda kichwani basi wewe ingia Google upate taarifa zaidi na kwa kina kumhusu huyo mgombea mwenza. Kama kizungu ni tia maji tia maji au hakipandi kabisa au umezoea kizungu cha ze ze zizi .basi wewe endelea kuniafuatilia nitakuwa nakuletea habari kwa undani.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.