POTOSHI Donald Trump, Rais wa Marekani amuwakia Bi Samia Suluhu Hassan

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Tunachokijua
Madai

Kupitia mtandao wa Youtube kuna video ikiwa na ujumbe unaosomeka Trump amuwakia Samia.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa madai hayo yanapotosha uhalisia kwani kilichoandikwa ni tofauti na kinachosimuliwa.

Kilichoandikwa ni kinaashiria Donald Trump amemuwakia Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, lakini kichosimuliwa ni tamko lilitolewa na ubalozi wa Marekani kuhusu kupitia upya ushirikiano wake na Tanzania.

Hivyo hakuna mahali ambapo Rais Trump alitamka yeye mwenyewe ama kuandika katika ukurasa wake kama ilivyo kawaida yake kumuwakia Rais wa Tanzania.

Tamko hilo lilitolewa na Naibu Msemaji Mkuu, Tommy Piggot liliambata na caption kupitia ukurasa wa intagram wa ubalozi wa Marekani Dar es salaam.


unajipa promo channel yako
 
Unatuona sisi mazwazwa...Mwambie Real DT tunamkaribisha aje awekeze mbugani Serengeti ajenge Hotel na Golf Course
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…