Miriam Mkanaka
Content Creator
- May 3, 2020
- 3
- 2
Kimsingi Mahakama ndiyo chombo pekee na cha mwisho cha utoaji haki katika Jamhuri ya Muugano wa Tanzania kama ilinavyoainishwa katika Ibara ya 107 (A) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara.
Ibara ya 13(6) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 iko wazi kwa Mtu Yoyote anayeshatikiwa kwa kosa la Jinai ana haki ya kutendewa kama mtu asiye anakosa mpaka mahakama itakapothibitishwa kuwa ana hatia (Pressumption of Innocence until proven guilty). Nukuu yake ni ifuatayo;
“Ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo’’.
Lakini pia ibara hiyo hiyo ya 13 (6) (b) inasema yafuatayo juu ya namna ya kuendesha mashauri ya jinai na madai mahakamani
"wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika"
Moja ya kanuni adhimu ya utoaji haki ni kwamba mtu yeyote yule asiadhibiwe bila kupewa fursa ya kujitetea/kusikilizwa, kisheria tunaita "Audi Alteram Partem" (The Right to be heard).
Katika kujitetea Sheria inatoa milango miwili ya mtu kutoa utetezi wake ambapo mlango wa kwanza ni mtu kujitetea yeye mwenyewe binafsi na mlango wa pili ni mtu kutetewa kwa uwakilishi yaani kupitia Wakili au Mawakili kadhaa.
Utetezi kupitia wakili upo kwa namna mbili, namna ya kwanza ni mtuhumiwa mwenyewe kwa uwezo wake wa kiuchumi ameamua kutafuta wakili kwa pesa yake yeye mwenyewe na kumlipa huyo wakili ili amtetee.
Kwa namna ya pili ni pale ambapo mtuhumiwa anapata Wakili kwa mujibu wa sheria, hapa nazungumzia Sheria ya Msaada wa Kisheria namba moja (1) ya mwaka 2017 chini ya vifungu vya 33-36 kwa msaada wa kisheria katika Makosa ya jinai.
Uwakilishi wa kwa mujibu wa sheria ni pale ambapo Mahakama kupitia kwa Msajili wa Mahakama Kuu anapoagiza Wakili yeyote aweze kutoa msaada wa kisheria na uwakilishi kwa mtuhumiwa mwenye uhitaji (Dock Brief) na zinafanyika sana.
Judge au Hakimu anayesikiliza kesi fulani na kwa kuungalia uzito wa kesi, adhabu itakayotolewa ikiwa mtuhumiwa atakutwa na hatia na kwamba mtuhumiwa hana uwezo wa kumlipa wakili, basi akiona hali hiyo Judge au Hakimu husika anatakiwa kuandaa cheti maalumu cha kuonesha kuwa mtu huyo ni mhitaji wa Wakili na cheti hicho kitapelekwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu kwaajili ya kumpatia mtuhumiwa huyo wakili, Msajili wa Mahakama Kuu ambaye hata hivyo ndiye anayetunza rejesta ya majina ya mawakili wote atapitia rejesta yake na kuchagua Wakili yeyote katika rejesta yake na kumuamru kwenda kumwakilishi mtuhumiwa ambaye ameonekana ana uhitaji wa uwakilishi.
Katika mazingira haya Wakili atalazimika kwenda kutoa utetezi kwa mtuhumiwa huyo bila kujali kama anataka au hataki na atatumia gharama zake yeye mwenyewe na mwisho wa kesi mahakama inaweza kutoa kifuta jasho ambacho mara nyingi hufikia laki mbili na elfu ishirini (220,000) na kama kuna pesa maalumu ulitumiwa unaweza kuzidai mahakamani.
Hivyo Mtuhumiwa anayo haki haki ya utetezi na kuwa na wakili, Pia kifungu cha 310 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022, kinaeleza kuwa kila mtu anayekabiliwa na mashtaka ya jinai katika mahakama yoyote ile, na hata mahakama ya mwanzo tangu 2022, ana haki ya kutetewa na wakili.
Zaidi Wakili ana wajibu wa kumhudumia mteja wa msaada wa kisheria kwa viwango sawa na yule aliyekulipa na ikitokea amefanya uzembe wowote au ameambiwa akafanye uwakili kwa mtuhumiwa mhitaji na akakataa basi atasimamishwa au kufutiwa kabisa uwakili wake kama ilivyotokea katika
kesi ya Wakili N.I.N MUNUO NGUNI Dhidi ya Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mwaka 1993. Wakili Munuo Nguni aliamriwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu kanda ya Arusha kwenda kuto msaada wa kisheria kwa mtuhumiwa wa mauaji mkoani Manyara (Babati) lakini Munuo alitakaa kwenda hivyo Jaji Mfawidhi alimsimamisha uwakili wake ndipo Munuo Nguni alipeleka kesi dhidi ya huyo Jaji Mahakama Kuu akipinga kusimamishwa uwakili wake.
Kwa upande mwingine kama kesi inamhusisha mtoto ni lazima apate msaada wa kisheria pasina kujali hali yake na hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 33 (2) cha Sheria ya Msaada wa Kisheria no. 1 ya mwaka 2017 (The Legal Aid Act).
Utaratibu huu wa kutoa msaada wa kisheria kwa watuhumiwa unafanywa pia na Chama cha Sheria cha Tanganyika kwa maana ya TLS kupitia Ofisi Kuu ya Dar es salaam na Ofisi Mikoani chini ya kamati maalumu ya msaada wa kisheria kwa umma, ambapo ikitokea mtu ameenda kuomba msaada katika ofisi hizo na akithibitika ni mhitaji kweli.
Wakili yeyote anaweza kuamriwa na kiongozi wa TLS Mkoa (Chapter Convenor) au Kamati ya Msaada wa Kisheria (Legal Aid Committee) kumwakilisha mteja huyo na atatakiwa kufanya hivyo pasina kujali anataka au hataki.
Mawakili katika kuchukua wateja wanaongozwa na kitu kinachoitwa "CABRANK RULE" kwa maneno mengine "THE RULE AGAINS'T DISCRIMINATION."
Hii ipo chini ya kanuni ya 140 ya Kanuni zinazoongoza ufanywaji wa kazi za kiwakili yaani THE ADVOCATES (PROFESSIONAL CONDUCT AND ETIQUETTE) REGULATIONS, 2018.
Hii Cab Rank Rule imetokana na neno CAB (ni American English) ambalo linamaanisha TAXI (kwa British English) na Teksi kwa Kiswahili.
Mawakili wanafananishwa na Madereva Teksi (Taxi/Cab drivers) kwamba hutakiwi kuchagua au kumbagua mteja anayetaka huduma.
Leo hii ukirequest usafiri wa Bolt au Uber dereva atakayekuja kukubeba hatakuuliza kuhusu tabia yako au kuacha kukubeba kwasababu ya tabia yako mbaya au nzuri ikiwa unamlipa.
Hii ni sawa na kazi za mawakili tabia yako au tuhuma zako sio kigezo cha yeye kukukataa. Ikiwa wakili atamkataa mteja kwa kigezo cha tabia au tuhuma zake basi wakili huyo anakuwa amekiuka maadili ya kazi za uwakili na anaweza kupewa adhabu ya mpaka kufutiwa uwakili wake na Kamati ya kitaifa ya maadili ya mawakili ikiwa atakutwa na hatia.
Wakili atamkataa mteja kwasababu kama vile pengine hana uzoefu na eneo la sheria ambalo mteja ametaka asaidiwe, mgongano wa maslahi baina yake na mteja, kama mteja anachotaka kipo kinyume na sheria, na kama mteja hana pesa ya kumlipa wakili.
Mwisho, japo sina uhakika ila unaweza kukuta hata hao mawakili wa akina nyundo wameamriwa na Msajili wa Mahakama Kuu kufanya uwakili au pengine ni akina nyundo au ndugu zao nyundo wamewatafuta au hao mawakili wenyewe wameamua kujitolea kuwasaidia.