Dondoo kuhusu kufanya biashara na mashirika ya serikali Tanzania

Dondoo kuhusu kufanya biashara na mashirika ya serikali Tanzania

Mike Twain

New Member
Joined
Aug 19, 2024
Posts
1
Reaction score
5
Kama mfanyabiashara wa Tanzania nikiwa na uzoefu wa takriban miaka 15, naomba nitoe uzoefu wangu kwa watu wanaotamani kuanza biashara zao wakilenga kupata tender za serikali kama source kubwa ya kipato.
Kila mteja ana changamoto zake kama wewe ni mfanyabiashara huitaj degree kujua ili, lakini ukimjua mteja wako itakusaidia ww kuyalinda maslahi yako inapokuja kwenye swala la kazi.

Lately kumekuwa na tuhuma nyingi kwa waasibu wa serikalini kuhusu kununua vitu kwa gharama kubwa ukilinganisha na bei halisi ya mtaani, kwa mfano tuseme mfuko wa cement mtaani unauzwa elf 17 lakini wanauziwa elf 32. Kwa jicho la kawaida utaweza sema kuna upigaji ila nataka tujifunze wote kwanini iko ivi.

Tip 1. Ukiwa unatender Mini-compettion make sure una multiply your price by 2 kusecure your actual profit. Mnaweza kusema ni wizi lakini take this in consideration. Lets say halmashauri ya Arusha ime nunua jenereta 2, na ww upo dar utasafirisha na kukabidhisha mzigo, ukiwapa mzigo watakudai risiti ili waprocess malipo kumbuka ukitoa risiti Tra wanakudai ela yao the next month na hawaelewi kama haujalipwa bado. na mara nyingi watu wa serikalini wanasogeza muda wa malipo kwa mfano kwenye tender document imeandikwa utalipwa within 30days, Lpo inatoka imeandikwa unalipa within 45 days alafu baada ya kuvutana kwingi wanakulipa after 80days na ukisema uwadai hela za kuchelewesha malipo mtaishia kupelekana mahakamani which ni kupoteza pesa tu.

Tip 2: ukiwa unatender National competition tenders, mara nyingi hizi tender zinakuwa na mikataba. jitahidi ukiwa unaweka bei Nest usiseme mzigo upo Tanzania quote kama mzigo ni wa kuagiza ila arrival time siku chache even if mzigo unao stock. then CIF amount weka ile amount nzima ya kununualia mzigo plus your 10% profit alafu the remaining amount ibaki uku kwenye landed cost then ukipata io tender mkisaini makubaliano waambie wakupe advance payment au ikibidi walipe in full kwasababu unaagiza nje, they usually accept ukiattach barua za manufacturer. why nakwambia ivi, hii inapunguza kadhia za kudai madeni kwa muda mrefu baada ya kumaliza kazi. watu hudai pesa zao mpka miaka 3 na wanalipwa bila penalties amount zozote kuongezwa (kwa wale wasio na misuli ya kupelekana mahakaman).

Tip 03: The best time kufanya kaz na watu waserikalini ni kuanzia mwez 9 mpka wa mwez wa 1, ichi kipindi kinachobakia nikipindi cha presentations na maombi ya kazi. why nakwambia ivi The government is ripe after mifumo ya pesa kufunguliwa na wanaanzaga manunuzi mwez wa nane kat kati apo na mpka inafika mwez wa 3 pesa nyingi zinakuwa zinaishilia so know your timings.

Nahisi nimefungua mwanga baadhi ya watu waliokuwa wakikata tamaa na hizi ishu.
 
Hivi huwa wanalipa kweli? Yani ukiweza kulipwa na serikali biashara nzuri lakini tatizo la serikali ni kulipwa. Serikali inazungusha sana, labda ufanye biashara ya cash, kama siyo hivyo mimi nilishindwa.
 
Kufanyakazi na serikali, kama ni kampuni changa..tena halmashauri huko, jiandae kufirisika kwa muda au kabisa
 
Mada nzuri ila hizo tender ni kama za ishu gani, embu nifafanulie kidogo mkuu.
 
Tender za serikali ni kujitafutia pressure tu.
 
Bi mkubwa wetu fulani alipata tender ya kupika chakula na kulisha moja ya mabwalo au mesi za jeshi fulani mkoani huko!

Alifanya kazi ya hiyo tender kwa miaka mitatu na nusu baadae akachoka sababu ya kuchelewa kulipwa malipo yake, wakati huo ana connection ya mume wake ni mstaafu wa hilo jeshi.

Kwa hiyo inategemea taasisi na aina ya tender, vinginevyo unaishia kupata sonona, presha au kisukari.
 
Back
Top Bottom