Mlo wa mchana huuongezea mwili nishati ya kuendelea kujiendesha kwa ufanisi mkubwa pasipo kukwama.
Ni msaada wa kipekee unaousukuma mwili katika kuendesha mifumo yake pamoja na kustahimili masaa ya mchana unapokuwa ofisini au nyumbani ukitelekeza majukumu yako.
Mpangilio wa sahani yako unapaswa kujali uwepo wa virutubisho muhimu kwa afya. Ili kurahisha mgawanyiko huu, unashauriwa kutenga
Nusu ya sahani iwe na mboga za majani na matunda.
Nusu nyingine inayobaki iwe na mchanganyiko wa vyakula vilivyotengenezwa kwa nafaka zisizo kobolewa pamoja na protini.
Nikila matunda tu mchana Inakuaje?
Yaan kila siku nakula matunda mfano, ndizi1, kipnde Cha tango, nanasi, tikiti, embe, apple, papai, chungwa1, nashusha Kwa pisi la mua, na nnashba je ntapata huo nishati thabiti!??
Ni ushauri mzuri but kwa wanaoishi mijini tena maeneo yao ya kazi huwezi mpangia mama ntilie akuwekee hiki na hiki may be watu wanaoishi vijijini hii wanaweza kutokana na huko kuna kila kitu.