Dondoo kuhusu ujenzi wa nyumba za kisasa

Dondoo kuhusu ujenzi wa nyumba za kisasa

samtz1

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2015
Posts
1,197
Reaction score
1,371
Kujenga nyumba yako mpya kunahitaji umakini mkubwa sana na wakati mwingine unahitaji kushiriki mwenyewe moja kwa moja katika nyanja zote za mchakato wa kujenga nyumba ili uhakikishe kuwa na mwisho mzuri wa nyumba yako "ya ndoto''.

Kumbuka kuwa nyumba yako utakayojenga inatarajiwa kukaa kwa muda mrefu hivyo basi kuna maamuzi mengi ambayo "lazima iwe" yafanywe na wewe.

Ikiwa hauwezi au haustahiki kufanya maamuzi haya, utawahimiza wajenzi wako kuhakikisha wanakupatia kitu kilichokuwa bora, chenye kwenda na wakati huku ukizingatia gharama nafuu na ubunifu unaoendana na wakati bila kusahau sheria na kanuni mbalimbali za ujenzi na taratibu za ki-nchi pia zifuatwe.

Tutaanza kwa kuangaza vitu 5 ambavyo unapaswa kujua na kuzingatia wakati wa kujenga nyumba yako mpya:-

1. Kujua gharama za ujenzi.
Kabla ya kuanza kujenga nyumba yako mpya, fanya tathmini na uweze kujua kama unaweza kumudu kujenga nyumba unayotaka, mfano, design ya nyumba na ukubwa wake na wapi inakwenda kujengwa, hii huweza kutoa gharama,na kukupa makadirio sahihi ya gharama za ujenzi, na mahesabu mengine yanayohusiana.

20160221_125116.jpg

b5b0d3d790f1d353cb1811d71a7af861.png

2. Angalia sifa ya wajenzi wako.
Wajenzi ni wengi na wote hawalingani wametofautiana kati ya mmoja na mwingine. Fanya uchunguzi mdogo wa kujua wajenzi wenye sifa nzuri kitaaluma. Ikiwa utaweza kutafuta habari mtandaoni au kupata mapendekezo kutoka kwa familia yako na marafiki, tafuta wajenzi wenye uwezo wa kufanya kazi bora na pia kwa wakati. Ni vizuri zaidi kutumia wataalamu wanaotambulika kisheria na bodi za ujenzi zilizopo hapa nchini kuepuka matatizo yakujengewa nyumba isiofuata kanuni na sheria za ujenzi.

Under_construction_Thai_modern_house.jpg

maxresdefault.jpg

3. Jenga kwa kuuza tena.
Haijalishi unapenda nyumba gani unayojenga, haitawezekana kuwa itakuwa nyumba ya mwisho utawahi kumiliki. Kujua kwamba, unapaswa kukumbuka thamani yake ya uuzaji na uwezo. Usiongeze mabadiliko mengi ambayo yatakuongezea gharama kwa baadae na kukupa wakati mgumu pindi utakapotaka kuiuza. Na usichague chochote pia nje ya kawaida. Jiulize ikiwa vipengele unayofikiria kufunga ni uwezekano wa kukata rufaa kwa wengine. Hii ni kwa mwenye mtazamo tu wakutaka kuja kuwa na nyumba nyingine kwa baadae kwani kwenye ujenzi kila siku huibuka mitindo mipya na baadhi ya watu hawapendi kupitwa na wakati.
PESA.jpg

4. Fikiria Kijani.
Hakikisha kufanya utafiti wako ili kuongeza ufanisi wa nishati katika kubuni nyumba yako mpya. Mjenzi wako na wajenzi wanaweza kukusaidia kuhakikisha kuwa madirisha yako yanakabiliwa na Kusini ili kupata jua kama iwezekanavyo inapojengwa nyumba yako. Utahitaji kuhakikisha kuwa bafu, sehem ya kufulia na gereji ni upande wa kusini wa nyumba yako na kuwa na madirisha madogo ili kupunguza kupoteza joto. Tumia muda kuchagua mifumo yako ya insulation na mifumo ya HVAC, pamoja na vifaa vya ufanisi vya nishati na mabomba ya maji na vumbi.
RX-DK-DIY020003_green-house-labeled_s4x3.jpg.rend.hgtvcom.1280.960.jpeg

5. Uchaguzi mzuri wa ‘finishing’ nzuri za nyumba yako

Watu wengi hufeli hapa unakuta nyumba imekuwa designed vizuri lakini inakuja kuharibiwa na finishing, kwa bahati dunia tunayoishi sasa imekuwa ni rahisi mno kujifunza kutoka kwa wengine na kuepukana na kuishi kimazoea. Finishing ya nyumba siyo tu muonekano lakini pia lazima kuzingatia vitu kama hali ya hewa na mazingira ya sehem husika mfano; kuna rangi maalum kwa ajili ya nje(exterior) na kuna rangi kwa ajili ya ndani yaani (interior) badala yake unakuta mafundi wetu wanachanganya ima kwa kutojua au kuzingatia matumizi vivyo hivyo hata kwenye aina zingine za materials zitumikazo kwenye ujenzi.

Muhimu ni kutumia wataalamu wa ujenzi ili kukukamilishia nyumba ''ya ndoto yako''

AHC%20-%204-%202.4%20mill%20-%20900sq.jpg

dawson-house--finished-pic---1_11304910.jpg

residential_interior_painting.jpg

cb-09-5631-008.jpg

15-kk-nagar-house-master-bedroom-3.jpg
 
Karibuni wadau pia michango ya wadau inaruhusiwa ili kila mmoja apate kujua nini afanye kabla ya kuchukua maamuzi ya kujenga nyumba
 
Mkuu bandiko murua sana! Ningeshauri Uwe una update kila mara. Vipi kuhusu matumizi ya nishati ya jua unashauri nini? Inawezekana ukatumia nishati ya jua kwa kila kitu.....fridge, AC, nk? Yaani mimi natamani tanesco nisideal nao kabisa.
 
Usijali nipo hapa kwa ajili hyo, nishati ya jua kwanza ni salama kwa matumizi, inawezekana kabisa kutumia nishati hii lakini itahitaji uandae bajeti kubwa ukilinganisha na umeme huu wakawaida wakati wa kuingiza ndani ya nyumba.
 
Kuna ile Channel ya Fine Living naangaliaga wenzetu hawana complications kwenye ujenzi ila wameongeza ubunifu zaidi..unakuta nyumba ya mbao lakini inavutia..ya kiaina tu lakini adabu..
 
Kuna ile Channel ya Fine Living naangaliaga wenzetu hawana complications kwenye ujenzi ila wameongeza ubunifu zaidi..unakuta nyumba ya mbao lakini inavutia..ya kiaina tu lakini adabu..
Watu wengi hudhani kutumia pesa nyingi kunnua materials (complex) kutaifanya nyumba yako ionekane nzuri, materials za kawaida kabisa zinatosha ukizingatia mpangilio mzuri wa nyumba
 
Umeandika vzuri sana. Ila umesahau ktu kimoja kushirikisha wataalamu wa ujenzi especially civil engineer. Watu wengi wanaojenga wanaona ubahili kumtafta engineer angalau ampe ushauri. Unakuta mtu anajenga nyumba zaidi ya milioni 80 ila kumpa engineer laki 5 kwa ajili ya ushauri anaona ubahili..
 
Kuna shida pia ya clients wengi kutojua kutofautisha watu wafuatao
1.Architects.
2.Civil/Structural engineers.
3.Quantity surveyors.
4.Electrical engineers.
5.Mechanical engineers.
6.na wengineo ambao sijawataja kama watu wa ICT. Hawa wote wanahusika kwenye ujenzi, mteja anachokijua yeye akimwachia fundi ujenzi kazi basi mchezo umeisha maana mafundi ndyo wanafahamika zaidi na wateja kwa hapa nchini kwetu kuliko hao nilowataja hapo juu
 
Watu wengi hudhani kutumia pesa nyingi kunnua materials (complex) kutaifanya nyumba yako ionekane nzuri, materials za kawaida kabisa zinatosha ukizingatia mpangilio mzuri wa nyumba
Kweli mkuu, hili tatizo linawakumba watu wengi wenye uelewa mdogo kuhusu ujenzi.
 
Kuna shida pia ya clients wengi kutojua kutofautisha watu wafuatao
1.Architects.
2.Civil/Structural engineers.
3.Quantity surveyors.
4.Electrical engineers.
5.Mechanical engineers.
6.na wengineo ambao sijawataja kama watu wa ICT. Hawa wote wanahusika kwenye ujenzi, mteja anachokijua yeye akimwachia fundi ujenzi kazi basi mchezo umeisha maana mafundi ndyo wanafahamika zaidi na wateja kwa hapa nchini kwetu kuliko hao nilowataja hapo juu
Pia hao ungewaongeza, ahsante kwa elimu nzuri
 
Back
Top Bottom